Habari za Punde

Mkutano wa Kampeni CCM Viwanja Vya Jumba la Vigae Urusi.

Mwanachama Mpya wa Chama cha Mapinduzi Ndg, Julius Mtatiro akisisitiza jambo wakati akihutubia katika Mkutano wa Kampeni wa Jimbo la Jangombe uliofanyika katika viwanja vya jumba la vigae Urusi Zanzibar akimpigia Kampeni Mgombea wa CCM Ndg Ramadhan Hamza Chande, kumpa ridhaa zao ili kutekeleza na kusimamia Ilani ya Uchaguzi ya CCM. 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Jangombe Zanzibar Ndg.Haji Ali akizungumza na kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Kichama Ndg. Juma Faki kuendelea na ratiba ya Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Uwakilishi wa CCM katika viwanja vya Jumba la Vigae Urusi Zanzibar.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mjini Kichama Ndg. Juma Faki akizungumza wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi Mgogo wa Jimbo la Jangombe Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya Jumba la Vigae Urusi akitowa maelezo ya Mgombea na kumuombea kura.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Unguja Kichama Ndg. Talib Ali Talib akhuutubia wakati wa Kampeni ya Uchaguzi Mdogo Jimbo la Jangombe katika viwanja vya Jumba la Vigae Urusi akimuombea Kura Mgombea wa CCM Ndg Ramadhan Hamza Chande, wakati wa mkutano huo na kumtambulisha Mgombea kwa Wananchi wa Tawi la CCM Urusi Unguja.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Kichama Ndg Talib Ali Talib akimtambulisha Mgombea wa CCM Ndg.Ramadhan Hamza Chande kwa Wananchi wa Shehia ya Urusi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya jumba la vigae urusi Unguja.

Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Ramadhan Hamza Chande akiwahutubia Wananchi wa Shehia ya Urusi wakati wa mkutano wake wa kampeni ya kugombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe na kuomba kura, kumchagua kuendelea na kuleta maendeleo kwa Wananchi wa Jimbo la Jangombe kutekeleza Ilani ya CCM kuwaletea maendeleo Wananchi.  


Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakiomba dua baada ya kumalizika kwa mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi wa Jimbo la Jangombe Zanzibar kupitia nafasi ya Uwakilishi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.