Habari za Punde

Mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya JKU na KMKM Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu Hizo zimetoka sare ya Bao 1-1.

Benchi la Ufundi la Timu ya JKU wakifuatilia mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar jana.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Katika mchezo uliokuwa na kila aina ya ufundi kuonesha nani zai na Timu ya KMKM ilijaribu kulipiza kisasi cha kufungwa na JKU katika mchezo wao wa Ufunguzi wa Ligi Kuu ya Zanzibar kuwania Ngao ya Hisani Timu ya KMKM ilikubali kipigo cha bao 1-0 na JKU kuibuka mshindi katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii uliofanyika Uwanja wa Amaan wiki iliopita.
Timu ya KMKM ilimeandia bao laki la kwanza katika kipindi cha Pili cha mchezo huo kupitia mshambuliaji wake Mussa Ali ameiandika bao hilo katika dakika ya  54 ya mchezo huo.
Nao Vijana wa JKU wakiwa katika harakati za kurejesha bao hilo kwa mashambulizi ya kustukiza wameweza kupata bao la kusawazisha katika dakika za nyongeza za mchezo huo katika kipindi cha pili kupitia mshambuliaji wake Rashid Abdallah akisawazisha katika dakika za nyongeza.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.