Habari za Punde

TAIFA STARS YAICHAPA CAPE VERDE 2-0 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika (AFCON) 2019 nchini Cameroon baina  ya Tmu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na Cape Verde  umemalizika katika  Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa wenyeji kutoka kidedea kwa mabao 2-0.
Taifa Stars wameshinda magoli mawili yaliyofungwa na mshambuliaji wa Difaa El Jadida ya Morocco Saimon Msuva katika dakika ya 29 akipokea pasi ya Mshambuliaji wa GRC Genk Mbwana Samatta. Mpaka Mapumziko Taifa Stars wanatoka kifua mbele kwa goli 1-0.

Katika kipindi cha Pili, Samatta aliipatia Taifa Stars goli la pili akimalizia pasi ya Mudathiri Yahya, akifuta lawama baada ya kukosa penati katika kipindi cha kwanza.

Taifa Stars walifanya mabadiliko ya kumtoa Abdi Banda na kuingia John Bocco, Mudathir nafasi yake ikichukuliwa na Feisal Toto.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.