Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limeteua kamati mpya ndogo ya wajumbe 10 watakao simamia soka la Zanzibar kwa muda mfupi.
Akizugumza na Wandishi wa Habari katika Ukumbi wa V.I.P wa uwanja wa Amaan Raisi wa Shirikisho hilo Wallace Karia amesema kamati hiyo itakuwa na jukumu la kusimamia upatikanaji wa Katiba ya ZFA, kushughulikia shughuli zote za ZFA za Kikatiba pamoja na kutayarisha Uchaguzi mpya kwaajili ya kupatikana viongozi wapya wa ZFA.
Karia amesema kamati hiyo wameiyunda baada ya vikao vya muda mrefu baina ya pande zote na kupata muafaka wa TFF kuunda kamati hiyo ambayo itafanya kazi zake hadi Novemba 30 mwaka huu.
..........CLIP... 1 KARIA...
Kuhusu suala la kamati ya iliounda mrajisi wa vyama vya michezo Karia amesema kamati hiyo kwa sasa haitofanya kazi tena baada ya TFF kuteuwa kamati hiyo ndogo na mazungumzo baina ya TFF na mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar yalifanyika na kufahamiana vizuri ambapo amewataja jumla ya wajumbe 10 wenye sifa na mapenzi ya Soka.
.........clip...2 Karia....
Baada ya kuundwa Kamati hiyo imezifuta kamati nyengine ndogo ndogo ikiwemo Kamati ya Soka la wanawake, Kamati ya Soka la Vijana (Central Taifa), Kamati ya Uchaguzi pamoja na Kamati ya Rufaa na Usuluhishi.
2 Attachments
|
TANTRADE YASHIRIKIANA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE KUTOA MAFUNZO YA UUZAJI
BIDHAA, UINGEREZA.
-
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTARADE) kwa kushirikiana na
Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Viwanda na Biashara Imeratibu Semina ya
Waf...
2 hours ago
Very Sad, ZFA tutafika kama hatuwezi kujiendesha mpaka muongozwe na watu wasiojua real situation on ground, Please stand for Zanzibar not personal Interests.
ReplyDelete