Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na mwenyejki wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta mjini Nairobi, Kenya
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta mjini Nairobi, Kenya
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein alisema kuwa Kenya na Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla zina uhusiano wa kihistoria na kindugu ambao ni lazima uimarishwe na uendelezwe kwa faida ya pande zote mbili.
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta mjini Nairobi, Kenya
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein alisema kuwa Kenya na Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla zina uhusiano wa kihistoria na kindugu ambao ni lazima uimarishwe na uendelezwe kwa faida ya pande zote mbili.
Dk. Shein aliyasema hayo wakati
akizungumza na Rais wa Kenya, Mheshimiwa
Uhuru Kenyatta katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta mjini Nairobi
.
Katika
mazungumzo hayo,Dk. Shein alisisitiza
juu ya ushirikiano katika kuendeleza uchumi wa bahari
kuu baina Kenya na Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla.
Dk. Shein alisema kwamba watu wa Tanzania ni ndugu na wamoja kwa hivyo ni muhimu pande mbili hizo
kuzidisha ushirikiano huo uliopo
katika masuala mbali mbali ya kiuchumi
na kijamii.
Akizungumzia
suala la kuendeleza uchumi wa bahari
kuu, Dk. Shein alishauri kwamba ni
muhimu kuandaliwe programu ya pamoja ya kuimarisha uvuvi wa bahari kuu, hatua ambayo ni muhimu katika jitihada
zinazoendelea za kukuza ajira kwa vijana
na kuwa na matumizi bora ya
rasilimali za bahari.
Vile vile,
katika kufanikisha mikakati na mipango iliyopo ya kuimarisha
matumizi bora ya rasilimali za bahari,
mito na maziwa alisema kwamba ni vyema nchi hizo zikahakikisha kwamba sekta
binafsi zinashirikishwa kikamilifu.
Aidha, Dk.
Shein alipendekeza kwamba itakuwa ni
vyema kuanzisha utaratibu ambao utaziwezesha timu za viongozi na wataalamu kutoka pande mbili hizo kukutana
mara kwa mara, ikiwa ni hatua muhimu ya
kujadili mafanikio na changamoto mbali
mbali zinazojitokeza katika sekta hiyo. Aliongeza kusema kwamba hatua
hiyo ni muhimu katika kuimarisha uhusiano uliopo.
Kwa upande
wake, Rais wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru
Kenyatta alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein na ujumbe aliofuatana nao kwa
kwa kukubali mwaliko wa kuhudhuria katika mkutano wa Kimataifa wa Uchumi
Endelevu wa bahari unaoendelea nchini
humo.
Rais Kenyatta alipongeza uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuanzisha
safari za meli baina ya Zanzibar na Mombasa kwa ajili ya kuimarisha huduma za
usafiri, biashara na kuendeleza uhusiano wa kidugu na kihistoria uliopo baina ya wananchi wa pande mbili hizo.
Vile vile, alishauri
kwamba itakuwa ni vyema hivi sasa kuimarisha huduma za usafiri kwa kuanzisha
safari za ndege za moja kwa moja baina
ya Zanzibar na Mombasa, ili kufanikisha
utekelezaji wa mipango na mikakati ya
kuimarisha sekta ya utalii, hasa ikizingatiwa kwamba sekta hiyo ni muhimu kwa
uchumi wa pande zote mbili.
Alisema kwamba hivi sasa wapo watalii
wengi wanaotembelea Mombasa ambao wangependa kusafiri moja kwa moja kwenda Zanzibar lakini
hushindwa kufanya hivyo kutokana na kukosekana kwa usafiri wa aina hiyo.
Mheshimiwa
Uhuru Kenyatta, alihimiza haja ya kuimarisha mikakati iliyopo ya kudhibiti
uvuvi haramu katika mwambao wa Afrika Mashariki, sambamba na kuimarisha hali ya usalama katika ukanda huo.
Katika kikao
hicho viongozi hao walikubaliana ziwepo ziara za mara kwa mara za viongozi wa
ngazi mbali mbali la kuongeza maelewano na kuhakikisha utekelezaji wa mambo
wanayokubaliana .
No comments:
Post a Comment