Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Shein, Ameondoka Nchini Kuelekea Nchini Kenya Kuhudhuria Mkutano wa Blue Economy.Akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Magufuli.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi na usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi na usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Salum Maulid Salum katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Wazee mbalimbali waliofika  katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Marubani wa Ndege ya Rais katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, kabla ya kuanza safari ya kuelekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.(Picha na Haroub Hussein)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ameondoka nchini leo kuelekea nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili.

Katika ziara hiyo Dk.Shein anamuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.

Akiongoza ujumbe wa Tanzania, Dk. Shein amefuatana na Viongozi mbali mbali wa Serikali za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo watahudhuria katika mkutano utaojalidi uchumi wa Bahari, utakaofanyika jijini Nairobi.

Mkutano huo unatarajiwa kuzishirikisha zaidi ya nchi saba Barani Afrika.

Katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, Dk. Shein ameagwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali, akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.

Abdi Shamnah, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: abdya062@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.