Wanachama hao waliosamehewa wakiwa wamesimama mbele ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu Mwenyekiti wake Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally na mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) wakati wa Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo tarehe Desemba 18, 2018 Jijini Dar es Salaam
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ofisi Ndogo ya
Makao Makuu Lumumba.
18 Desemba, 2018
Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa kimefanyika leo tarehe 18 Desemba, 2018 Jijini Dar es Salaam na
kuongozwa na Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kikao hicho kimepokea taarifa ya
utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na
taarifa ya chama juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa CCM ya
mwaka 2015.
Pia, kikao hicho kimepokea taarifa
kuhusu masuala ya maadili, kimepokea na kuridhia marekebisho ya kanuni mpya za
fedha na mali za chama na jumuiya zake na kimepokea na kuridhia uteuzi wa
wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM.
Kwa kauli moja Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa imepokea maombi na kukubali kusamehewa adhabu ya kufukuzwa uanachama
kutoka kwa waliokuwa wana CCM wanne ambao walitenda makosa hayo wakiwa
Wenyeviti wa CCM ngazi ya Mikoa na Wilaya.
Waliosamehewa na kurejeshewa uanachama
ni;
1.
Ndg.
Ramadhani Rashid Madabida (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam).
2.
Ndg.
Erasto Izengo Kwirasa (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga).
3.
Ndg.
Christopher Mwita Sanya (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara).
4.
Ndg.
Salum Kondo Madenge (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni).
Aidha, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa
kauli moja imeamua kumuweka katika uangalizi Ndg. Jesca Msambatavangu ambaye
ameomba kurejeshewa uanachama wa CCM baada ya kufukuzwa kwa makosa ya
kimaadili.
Halikadhalika, Halmashauri Kuu ya CCM
imepitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama
katika ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa zilizoachwa wazi baada ya waliokuwa
katika nafasi hizo kupangiwa majukumu mengine ya Kiserikali au kufariki dunia pamoja na mgombea wa CCM wa
kiti cha Ubunge katika Jimbo la Temeke Jijini Dar es Salaam.
Waliopitishwa kugombea nafasi hizo ni
kama ifuatavyo.
1.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
i.
Dkt.
Damas Mukasa Kashegu
ii.
Asha
Juma Feruzi
iii.
Galila
Ramadhani Wabanhu
iv.
Makene
Pamella Boniphas
2.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Iringa
i.
Dkt.
Abel Mwendawile
ii.
Aman
Said Mwamwindi
iii.
Sabas
Vitus Mushi
3.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi Mkoa wa Simiyu
i.
Mashaka
Abeid Makongoro
ii.
Mayunga
Genga Ngokolo
iii.
Heri
Mchunga Zebedayo
4.
Mwenyekiti
wa Wazazi Mkoa wa Mwanza
i.
Bahebe
Emmanuel Ezekiel
ii.
Nyiriza
Makongoro Nyiriza
iii.
Masso
Gerald Jane
iv.
Misogalya
Isaac Kilangi Kassile
5.
Mwenyekiti
wa Wazazi Mkoa wa Mwanza
i.
Salum
Mohamed Chima
ii.
Yusuph
Mwandami Gwayaka
iii.
Bertha
Peter Nakomolwa
iv.
Philemon
Josephat Kiemi
6.
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini
i.
Amina
Ally Kobo
ii.
Lemmy
Joel Ludovick
iii.
Hamidi
Rajabu Shebuge
Halmashauri Kuu ya CCM imemteua Ndg.
Abdallah Ally Mtolea kuwa Mgombea wa kiti cha ubunge kwa tiketi ya CCM katika
Jimbo la Temeke, Jijini Dar es Salaam.
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imeiagiza
Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) kurudia mchakato wa kupendekeza majina ya
mgombea wa nafasi ya Mjumbe wa NEC.
Wakati huo huo, Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa kwa kauli moja imetupilia mbali pingamizi zilizowekwa dhidi ya viongozi
wa CCM katika ngazi mbalimbali na kuagiza viongozi hao waendelee na nyadhifa
zao.
Pingamizi hizo ziliwekwa dhidi ya
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndg. Anthony Mwandu Diallo, Mwenyekiti wa
Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Lindi Ndg. Aisha Ally, Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Ndg. Salim Mohamed na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngara Ndg. George
Jackson Rubagora.
Pamoja na kutupilia mbali pingamizi
hizo, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imewaagiza walezi wa mikoa yote ambayo viongozi
wake waliwekewa pingamizi wakutane na wanachama na kukiunganisha chama.
Halmashauri Kuu ya CCM imemuagiza Ndg.
Zubeir Majaliwa (aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Uvinza) ambaye
Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Uvinza ilimsimamisha uanachama kuwasilisha rufaa
yake kuanzia ngazi husika wakati adhabu yake ikiendelea.
Aidha, Halmashauri Kuu ya CCM imetoa
adhabu ya KALIPIO kwa mwanachama wa CCM Ndg. Hasnain Murji kutokana kukabiliwa
na makosa ya kimaadili.
Ndg. Bashiru Ally Kakurwa
Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI.
No comments:
Post a Comment