Habari za Punde

Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Aapishwa leo.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye (kushoto) akimvua cheo cha zamani na kumvisha cheo kipya cha Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Mbaraka Semwanza katika ukumbi wa mikutano Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi Dar es salaam mapema leo asubuhi tarehe 11/12/2018
Kamishna (CF) Mbaraka Semwanza akiapa baada ya kuvishwa cheo kipya cha Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi
Kamishna wa Utawala na Fedha (CF) Mbaraka Semwanza (kushoto) akipokea nyaraka mbalimbali za ofisi ya Utawala na Fedha kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye (kulia), baada ya kuapishwa katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi
 Makamishna, Wakuu wa Vitengo, Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakishuhudia kuapishwa kwa Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi 


NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.