Habari za Punde

Mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo.

Na Takdir Ali,                                    

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ofisi ya Zanzibar Tunu Juma Kondo amewataka Wanawake wenzake kushirikiana katika  kukuendeleza mipango ya kuimarisha Jumuiya yao na kuweza kukipatia ushindi Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020.
Amesema Wanawake wanamchango mkubwa katika katika kuleta maendeleo na ushindi wa Chama hivyo hakuna budi kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuweza kukipatia ushindi chama hicho.
Tunu Ameeyasema hayo huko Afisi ya CCM Kisiwanduwi katika sherere ya kupokelewa kufuatia kuteuliwa nafasi hiyo hivi karibuni.
Ameeleza kuwa Wanawake wanahaitaji kupendana,kuepukana na Majungu,Fitna na Uhasama ili kuhakikisha wanaleta maendeleo kwa wanachama wanawaongoza na kuweza kujiletea maendeleo.
Aidha amewataka kutumia hekima na busara katika Uongozi wao ili mipango ya maendeleo iliopangwa ikiwemo kupiga vita Udhalilishaji na Rushwa ili iweze kufikiwa katika maeneo yao.
Amefahamisha kuwa viongozi wanawajibu wa kuwahudumia Wanachama wao kwa lengo la kuwahamasisha Vijana kuweza kujiunga kwa wingi katika Umoja huo.
Nao baadhi ya Wanachama wa UWT,Zanzibar wamepongeza Naibu Katibu Mkuu huyo kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kuahidi kushirikiana katika kufanya kazi kwa ufanisi ili kuweza kufikia malengo yaliopangwa.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.