Habari za Punde

MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM TAIFA AKUTANA NA KAMATI YA SIASA MKOA WA PWANI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge  wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Francis Koka pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya utambulisho kama Mlezi wa Chama hicho mkoa wa Pwani
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Kibaha mjini Bi. Azilongwa Bohari pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya utambulisho kama Mlezi wa Chama hicho mkoa wa Pwani
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndugu Ramadhani Maneno (kulia) akimtambulisha Mlezi wa CCM mkoa huo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Taifa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani mara baada ya kujitambulisha rasmi kama Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani, hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya mji Kibaha

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.