Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (R), SemistoclesKaijage akitoa taarifa kwa umma kuhusu Uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Temeke na Udiwani katika kata 46 za Tanzania Bara
Na. NEC. 7
Desemba 2018.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo
katika Jimbo la Temeke, Mkoani Dar es Salaam na kwenye Kata 46 za Tanzania
Bara.
Akitangaza kufanyika
kwa uchaguzi huo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (Rufaa),
Semistocles Kaijage amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika Januari 19 mwaka 2019 na
fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 20 Desemba
2018.
"Uteuzi wa Wagombea
utafanyika tarehe 20 Desemba, mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya
tarehe 21 Desemba, hadi tarehe 18 Januari, mwaka 2019 na siku ya
uchaguzi itakuwa
ni tarehe 19 Januari mwaka 2019,” amesema Jaji Kaijage.
Jaji Kaijage
amebainisha kuwa Tume imetangaza uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo la
Temeke baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai juu ya
uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika jimbo hilo.
Amesema kuwa Tume ilipokea
barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia
kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, aliitarifu Tume
uwepo wa nafasi wazi ya Mbunge wa Jimbo la Temeke katika Halmashauri ya Wilaya
ya Temeke Mkoani Dar es Salaam kufuatia Kujiuzulu uanachama wa Chama Wananchi
CUF kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Maulid Said Abdllha Mtolea.
Kwa upande wa nafasi wazi
za Udiwani Jaji Kaijage amesema kuwa Tume
ilipokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali ya Mtaa akiitaarifu
Tume juu ya uwepo wa nafasi wazi za
Udiwani katika Kata 46.
“Tume imepokea Taarifa
kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaaa mbaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa,
Sura ya 292, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 46 za
Tanzania Bara,” amesisitiza Jaji Kaijage.
Ametoa wito kwa vyama
vya siasa na wadau
wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu,
Miongozo na maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa
kipindi cha Uchaguzi mdogo.
Jaji Kaijage
amefafanua kuwa kuwa uchaguzi huo mdogo utafanyika ndani ya Halmashauri 28 zilizopo
kwenye Mikoa 14 ya Tanzania Bara.
Halamashauri na Kata zitakazokuwa
na Uchaguzi ni pamoja na Ngorongoro (Sale,Misigyo,Malambo,
Orgosorok na Olorien/Magaiduru), Arusha(Kimnyak),
Kilwa (Kiranje ranje, Kikole, Pande
Mikoana), Liwale (Kata Kichonda na
Mlembwe), Babati(Dareda na Magara, Kiteto(Makame), Simanjiro(Loiborsiret, Ruvu Remit, Naberera), Kwimba(Walla), Sengerema(Nyampulukano), Ulanga(Msogezi), Mvomero(Mtibwa, Tchenzema, Mangae), Kilosa(Magomeni), Temeke(Keko), Kinondoni(Magomeni).Halmashauri nyingine ni
pamoja na Kasulu (kata ya Kitanga), Kasulu Mji( Kata za Kigondo na
Msambara), Buhigwe(Mnyegera), Bukoba(Buhendagabo, Nyakato, Kikomelo),
Misenyi(Kanyigo), Ngara(Nyamiaga),
Mbinga(Utiri), Songea(Mpitimbi), Mbozi(Ilolo, Hasanga, Ihanda), Tandahimba(Nahyanga,
Namikupa), Dodoma(Dodoma Makulu), Serengeti(Geitasamo), Bariadi(Nkundwabiye) na Bariadi Mji(Nyangokolwa).
Caption
Picha – 1. Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (R), SemistoclesKaijage akitoa taarifa
kwa umma kuhusu Uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Temeke na Udiwani katika kata
46 za Tanzania Bara
No comments:
Post a Comment