Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina(kushoto), akimsikiliza Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Ki-TANESCO Mirerani, Mhandisi Zacharia Masatu, akifafanua kuhusu namna TANESCO ilivyoweza kufikisha umeme wa kutosha kwenye eneo la Mirarani leo Januari 21, 2019.
Na.Mwandishi Wetu. Mirerani.
UWEKEZAJI
kwenye miundombinu ya umeme uliofanywa na Serikali kupitia Shirika la Umeme
Tanzania TANESCO umeanza kuzaa matunda eneo la machimbo ya madini Mirerani
mkoani Manyara.
Serikali
kupitia TANESCO iliwekeza kwa kujenga kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha
KIA na hivyo kuwezesha hali ya upatikanaji umeme ulio bora na wa uhakika kwenye
eneo la Mirerani kuongezeka.
Kwa
sasa matumizi ya umeme kwenye eneo lote la Mirarani ni kiasi cha Megawati 3.5
lakini kubwa zaidi miongoni mwa watumiaji wakubwa walioanza kufaidika na
uwekezaji huo ni pamoja na kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe
(Graphite) na kile cha Mirerani Tanzanite vyote viko Mirerani.
Meneja
wa Shirika la Umeme wilaya ya Ki-TANESCO Mirerani Mhandisi Zacharia Masatu amewaambia
waandishi wa habari wanaotembelea eneo hilo kuwa kiwanda hicho pekee kinatumia
kiasi cha Megawati 1.1 ya umeme.
Aidha
Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina amesema jiji lina ziada
ya umeme Megawati 50, na hivyo amewahimiza wawekezaji katika sekta ya viwanda
vikubwa, vya kati na vidogo kuwekeza ili kufaidi uwekezaji wa serikali katika
miundombinu ya umeme nchini.
“Wito wetu kwa wafanyabiashara na wawekezaji,
waje wawekeze kwenye mkoa wetu wa Arusha sababu kama tulivyoeleza awali tuna
umeme wa kutosha, kwa mkoa mahitaji ni Megawati 75 na uwezo wa kituo chetu ni
Megawati 120 kwahiyo unaweza kuona tuna
ziada inayofikia Megawati 50.” Alisema Mhandisi Mhina.
Mhandisi
Mhina alibainisha kuwa, viwanda vinaweza kuleta matokeo makubwa ya uwekezaji katika
miundombinu ya umeme uliofanywa na serikali kwani matumizi ya kiwanda kimoja
inaweza kuwa ni mahitaji ya wilaya
nzima.
“Viwanda
ni njia mojawapo inayoweza kutupeleka kwenye uchumi wa kati tunaotaka kwa
haraka zaidi.” Alisisitiza.
TANESCO ilifunga mitambo ya kuingiza umeme wa kutosha
kwenye kiwanda cha Godmwanga Gems Limited na kwamba kinajitegemea ambapo kuna jumla ya transfoma
pozo kubwa tatu na gharama za ufungaji wa mitambo hiyo zinakadiriwa kufikia
shilingi Milioni 60.
Aidha
afisa wa kiwanda hicho cha kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (graphite), Nai
Mainga alisema kiwanda kilianza uzalishaji wa madini hayo ya graphite (kinywe) Juni 2018 na kwamba
tangu uzalishaji uanze hadi hivi sasa, tayari wamezalisha kiasi cha tani 5,600
na wateja wakubwa wa madini hayo ni China.
“Matumizi
makubwa ya madini hayo ya kinywe hutumika kutengeneza vitu maka betri na
tunapozungumzia betri ni pamoja na betri zile kubwa za magario na mitambo,
lakini pia kuna taarifa kuwa madini hayo hutumika kutengeneza bati maalum la
kuzuia injini ya ndege ili isipate moto sana kwani madini haya huchomwa sana
ili kupata zao la mwisho.” Alifafanua.
Alisema
kuna baadhi ya nchi ambazo tayari zimeanza mchakato wa kusitisha matumizi ya petrol
kuendeshea magari na hivyo kuna uwezekano wa kutumia madini haya ili
kutengeneza betri za kuendesha magari.
![]() |
Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina |
Kituo cha kupokea umeme kilichoko ndani ya kiwanda cha kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe, (graphite) huko Mirerani mkoani Manyara ambapo TANESCO imefu nga mitambo na transfoma kubwa tatu ili kutoa umeme toshelezi kwa kiwanda hicho.
Kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe
(Graphite)
Kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe
(Graphite)
Mhandisi Zacharia Masatu, akifafanua jambpo ndani ya kituo cha kupokelea umeme kwenye kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe
(Graphite)
No comments:
Post a Comment