Habari za Punde

Kamati BLW Ofisi za viongozi wakuu ziarani Pemba

 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed, akizungumza na watendaji wa  vitengo kutoka Wizara  yake na Wajumbe wa kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati walipofanya ziara katika Ofisi hiyo Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 BAADHI ya Wajumbe wa kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi zanzibar, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Mohamed Aboud Mohamed, kabla ya wajumbe wa kamati hiyo kuangalia miradi mbali mbali inayotekelezwa na Ofisi hiyo Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MRATIB wa TASAF Pemba Mussa Said akitoa maelezo juu ya kikundi cha walengwa wa kaya masikini Jambonia kinachojishuhulisha na utengenezaji wa sabuni za michi, kilichopo Jambangome Shehia ya Mzingani Wilaya ya Mkoani, wakati wajumbe wa kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati walipotembelea kikundi hicho katika ziara yao ya kuangalia miradi ya maendeleo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MWENYEKITI wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambaye pia ni mwakilishi wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Unguja Panya Ali Abdallah, akinunua sabuni za michi kwa kikundi cha Walengwa wa kaya masikini Cha Jambonia kilichopo Jambangome Wilaya ya Mkoani, wakati wajumbe wa kamati hiyo walipokitembelea kikundi hicho katika ziara yao Kisiwa Pemba(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 FISA Tume ya Uchaguzi Wilaya ya Chake Chake Othaman Khamis Othaman, akisoma taarifa ya tume ya Uchaguzi kwa wajumbe wa kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, huu baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakipitia taarifa hiyo kwa umakini mkubwa, wakati kamati ilipofika kuangalia utendaji kazi wa tume hiyo(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.