Habari za Punde

TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2018 KWA SKULI ZA ZANZIBAR.1.0 UTANGULIZI
Kwa heshima naomba kuwasilisha Taarifa kuhusu Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2018 kwa Skuli za Sekondari za Zanzibar. Taarifa hii inafanya pia ulinganisho na matokeo kama hayo na Skuli za Tanzania kwa ujumla. Pia taarifa hii italinganisha matokeo ya mtihani kama huo kwa mwaka 2017.

2.0 UANDIKISHAJI WA WATAHINIWA
Mtihani wa Kidato cha Nne, mwaka 2018, ulifanyika nchini kote kuanzia tarehe 05/11/2018 hadi 23/11/2018. Jumla ya watahiniwa 426,988 waliandikishwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 219,171 (51.33%) na wavulana 207,817(48.67%).  

Kwa upande wa skuli za Zanzibar, jumla ya watahiniwa 17,098 waliandikishwa kutoka skuli 213, kati ya hizi skuli 164 ni za Serikali ambazo zimeandikisha wanafunzi 15,168 na skuli 49 ni za Binafsi ambazo zimeandikisha wanafunzi 1,930. Jumla ya wanafunzi 16,654 walifanya mtihani mwaka 2018 sawa na asilimia 97.4 ya watahiniwa walioandikishwa kati yao 9,886 ni wasichana sawa na asilimia 59 na watahiniwa 7,212 ni wavulana sawa na asilimia 43.3. Aidha, jumla ya watahiniwa 444 sawa na asilimia 2.6 ya watahiniwa walioandikishwa hawakufanya mtihani.

3.0 MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2018
Jumla ya watahiniwa 322,965 sawa na asilimia 78.38 ya watahiniwa waliofanya mtihani kwa Tanzania nzima wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 163,920 sawa na asilimia 77.58 wakati wavulana ni 159,045 sawa na asilimia 79.23. Kwa ujumla, asilimia ya ufaulu imeongezeka kwa 1.29 ukilinganisha na asilimia 77.09 ya mwaka 2017.  

Kwa upande wa Skuli za Zanzibar, watahiniwa 16,654 sawa na asilimia 72.7 ya watahiniwa wote wa skuli za Zanzibar wamefaulu. Kwa ujumla asilimia ya ufaulu imeongezeka kwa asilimia 1.9 ya mwaka 2017. 

JADWELI NA 1: MADARAJA YA UFAULU

DARAJA TANZANIA ZANZIBAR
 IDADI ASILIMIA IDADI ASILIMIA
I 13,524 3.77 225 1.4
II 39,665 11.07 997 6.0
III 60,636 16.92 2,039 12.2
I – III 113,825 31.76 3,261 19.6
IV 170,301 47. 51 8,845 53.1
I – IV 284,126 79.27 12,106 72.7
0 74,301 20.73 4,548 27.3
  
4.0 UFAULU KIMASOMO
Takwimu za matokeo zinaonesha kuwa ufaulu katika masomo ya Historia, Kiswahili, Hesabati, Physics, Chemistry na Book-keeping umepanda kati ya asilimia 0.83 hadi 8.76 ikilinganishwa na mwaka 2017.  
Watahiniwa wengi wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili sawa na asilimia 89.32.  Aidha, ufaulu wa chini kabisa ni wa somo la Hesabati ambapo ni asilimia 20.02 tu ya wanafunzi wote wa skuli walifanya somo hilo wamefaulu. 

Mchanganuo wa ufaulu kimasomo katika mtihani wa Kidato cha Nne 2018 ukilinganisha na mwaka 2017 unaonekana katika jadweli lifuatalo: -

JADWELI NA 2: ASILIMIA YA UFAULU KWA MASOMO

 WALIOFAULU 2018 WALIOFAULU 2017
 ASILIMIA ASILIMIA
CIVICS 57.25 58.75
HISTORY 57.29 55.99
KISWAHILI 89.32 84.42
ENGLISH 66.30 67.86
GEOGRAPHY 53.03 53.18
BIOLOGY 60.89 61.37
CHEMISTRY 62.15 53.39
PHYSICS 45.50 42.17
BASIC MATHEMATICS 20.02 19.19
COMMERCE 42.66 46.45
BOOK-KEEPING 44.67 40.82

Skuli zetu za Mikunguni na Lumumba zimeonesha ufaulu mzuri kwa baadhi ya masomo kwa upeo wa Tanzania.

Lumumba Sekondari

Dini 8/1045 Physics 20/ 4539 Chemistry 26/4784
Mikunguni Sekondari

Workshop technology 1/10 Electrical installation 1/10 Fitting and turning 1/10 Electrical Drafting 1/10
Building construction 2/10 Carpentry and joinery 2/10 TV and radio service 2/10 Mechanical drafting 2/10

5.0 SKULI KUMI BORA NA SKULI KUMI ZA MWISHO
Ubora wa skuli   umepangwa kwa kutumia kigezo cha wastani wa pointi (Grade Point Average – GPA) katika ufaulu wa masomo kwa wanafunzi katika skuli ambapo mchanganuo ni A=1, B=2, C=3, D=4 na F=5.  

Kwa upande wa Zanzibar skuli kumi bora zilizokuwa na wanafunzi 40 au zaidi ni hizi zifuatazo: -

NAFASI JINA LA SKULI IDADI YA WATAHINIWA MKOA
1. LUMUMBA 112 MJINI/MAGHARIBI
2. FIDEL CASTRO 67 KUSINI PEMBA
3. LAUREATE INT. 48 MJINI/MAGHARIBI
4. TUMEKUJA  122 MJINI/MAGHARIBI
5. SOS  55 MJINI/MAGHARIBI
6. HIGHVIEW 57 MJINI/MAGHARIBI
7. MAHAD ISTIQAMA 44 KUSINI UNGUJA
8. MIKUNGUNI 48 MJINI/MAGHARIBI
9. GLOURIOUS ACADEMY 72 MJINI/MAGHARIBI
10. WETE SECONDARY 60 KASKAZINI PEMBA

Skuli za mwisho zenye watahiniwa zaidi ya 40 kwa Zanzibar ni hizi zifuatazo:

NAFASI JINA LA SKULI IDADI YA WATAHINIWA MKOA
1. P/MCHANGANI 60 KASKAZINI UNGUJA
2. UKUTINI 51 KUSINI PEMBA
3. KIJINI 55 KASKAZINI UNGUJA
4. NG’AMBWA 101 KUSINI PEMBA
5. HAMAMNI 175 MJINI MAGHARIBI
6. KANGAGANI 50 KASKAZINI PEMBA
7. WAMBAA 56 KUSINI PEMBA
8. KENGEJA 80 KUSINI PEMBA
9. DONGE 124 KASKAZINI UNGUJA
10. KINOWE 64 KASKAZINI PEMBA

5.1  WATAHINIWA 10 WA ZANZIBAR WALIOFANYA VIZURI ZAIDI MWAKA 2018
    WANAFUNZI KUMI BORA 
S/N JINA LA MWANAFUNZI JINSIA ALAMA SKULI
1 HASSAN HAMID USSI M 7 LUMUMBA
2 YAHYA ALI HEMED M 8 LUMUMBA
3 YUSSUF UBWA MOHAMMED M 9 LUMUMBA
4 MOHAMMED ABDALLA MBAROUK M 9 LAUREATE
5 FAIZA SULEIMAN KHAMIS F 10 LUMUMBA
6 HIDAYA SAID RASHID F 11 LUMUMBA
7 ALI JUMA SAID F 11 LUMUMBA
8 MOHAMMED FADHIL JUMA M 11 LUMUMBA
9 HASSAN MRISHO SHARIA M 11 JKU
10 SAID MBAROUK SHEBA M 11 JKU

6.0  TATHMINI YA JUMLA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE  2018
Matokeo ya jumla ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2018 ya watahiniwa wa skuli yanaonesha kuwa ufaulu kwa jumla umeongezeka kwa asilimia 1.29 kutoka asilimia 77.09 mwaka 2017 hadi asilimia 78.38 mwaka 2018. Aidha, takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa daraja la I-III imeongezeka ambapo mwaka wa 2016 ilikua ni asilimia 27.60, mwaka 2017 asilimia 30.15 na mwaka 2018 imekua ni 31.76. Kwa upande wa Zanzibar takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa daraja la I-III imeongezeka kutoka asilimia 18.8 mwaka 2017 na kufikia asilimia 19.6 mwaka 2018. 

Pamoja na kuongezeka kwa asilimia ya ufaulu, takwimu zinaonesha kuwa ufaulu wa masomo ya Physics, Basic Mathematics, Commerce na Book-keeping upo chini ya asilimia hamsini (50%).

Hakuna tokeo lolote la kufutwa au kuzuiliwa matokeo ya mitihani katika skuli za Unguja na Pemba.

9.0 HITIMISHO
Matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne ya mwaka 2018 kwa skuli za Zanzibar ni ya wastani.  Idadi ya watahiniwa waliopata sifa za kujiunga na masomo ya Kidato cha Tano na Taasisi ya Ufundi ya Karume imeongezeka kutoka 3,033 (2017) hadi 3,261 (2018).

Hata hivyo idadi ya wanafunzi waliofaulu kwa madaraja ya kwanza hadi tatu ni ndogo (19.6%) ikilinganishwa na wale wanaofaulu kwa daraja la nne (53.2%). Hali hii imepelekea mikoa ya Zanzibar kuwa ya mwisho katika wastani wa ufaulu kwa upeo wa Tanzania.

Wizara itaendelea na juhudi zake za kuzipatia skuli vifaa vya kufundishia pamoja na kuajiri walimu wenye sifa ili kuinua kiwango cha ufaulu.

Aidha, Wizara inaendelea kuwaomba wazazi na jamii kwa jumla kuendelea kushirikiana nasi katika kufuatilia maendeleo ya Watoto ili lengo la Wizara la kutoa elimu bora lifikiwe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.