Habari za Punde

TANESCO Yawahimiza Wawekezaji Kuwekeza Kwenye Viwanda,Umeme Bora na wa Uhakika Upo wa Kutosha.


 Picha ya dron ikionyesha muonekano wa sasa wa mitambo ya kufua umeme wa gesi Kinyerezi II jijini Dar es Salaam. Mradi huo umekamilika na unafua umeme wa Megawati 240.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Nchini TANESCO limewahimiza wananchi kuwekeza kwenye viwanda kwani hivi sasa umeme bora na wa uhakika upo, Meneja Miradi wa Shirika hilo, anayeshughulikia uzalishaji (Generation) Mhandisi Stephene S. A. Manda (pichani juu) amesema leo Januari 9, 2019. Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea utekelezaji wa miradi ya umeme Kinyerezi II wa Megawati 240 na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I wa Megawati  185. “Mradi wa Kinyerezi namba II wa Megawati 240 umekamilika, kwa hivyo ombi letu kwa wote ambao wanaweza kuwekeza kwenye viwanda wawekeze kwani umeme wa uhakika na wa kutosha  upo.” Alisema na kuongeza. Licha ya mradi huo wa Kinyerezi II Mradi mwingine ni wa upanuzi wa Kinyerezi I unaozalisha megawati 150 ili ufikie Megawati 335 kwa kuongeza Megawati 185.“Itakapofika Agosti 2019 jumla ya umeme utakaokuwa unatoka Kinyerezi pekee ni Megawati 575 kwa hivyo ni umeme wa kutosha, kama ni kulisha Dar es Salaam, basi Dar es Salaam nzima Kinayerezi inaweza kuibeba.” Alitoa hakikisho. Kwa hivyo uwezo wa kuhakikisha viwanda vinapata kile vinavyopasa kupata kuhusiana na umeme TANESCO imejipanga vizuri na tunaomba sana wawekezaji wawekeze, kiwanda si lazima kiwe kikubwa sana, hata cha kukoboa na kusaga nafaka na vile vya kukamua matunda ya kutoka Tanga na kwingineko. Alisema Mhandisi Manda. Alitoa wito kwa watanzania kuuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kujenga uchumi wa kati na wa viwanda kwani inawezekana kwa vile umeme upo, ulio bora na wa uhakika.
 Picha ya dron ikionyesha muonekano wa sasa wa mitambo ya kufua umeme wa gesi Kinyerezi II jijini Dar es Salaam. Mradi huo umekamilika na unafua umeme wa Megawati 240.
Meneja Miradi wa Shirika hilo, anayeshughulikia uzalishaji (Generation) Mhandisi Stephene S. A. Manda, akiwa kwenye chumba cha udhibiti mitambo (control room) cha kituo cha kufua umeme wa gesi Kinyerezi II leo Januari 9, 2019.

 Mhandisi Stephene S. A. Manda (katikati), akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Miradi wa kampuni ya Jacobsen Elektro Ingar Tollum Andersen (kulia) na Mtaalamu wa kusimika mitambo kutoka kampuni hiyo, Markku Siren wakati alipotembelea kuona maendeleo ya mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I leo Januari 9, 2019.
 Picha ya dron ikionyesha muonekano wa sasa wa mitambo ya kufua umeme wa gesi Kinyerezi II jijini Dar es Salaam. Mradi huo umekamilika na unafua umeme wa Megawati 240.
  Picha ya dron ikionyesha muonekano wa sasa wa mitambo ya kufua umeme wa gesi Kinyerezi II jijini Dar es Salaam. Mradi huo umekamilika na unafua umeme wa Megawati 240.
 Mhandisi Manda akiwa juu kabisa ya jengo la utawala la Kinyerezi II, akifafanua kukamilika kwa mradi huo ambapo amesema kazi iliyobaki ni kuimarisha bustani na kusafisha njia.
 Jengo la utawala Kinyerezi II kama linavyoonekana leo Januari 9, 2019.
 Jengo la karakana na ghala la vifaa.
 Mhandisi Manda akionyesha moja ya mashine mpya zilizoko kwenye karakana ya Kinyerezi II.
 Meneja wa Kituo cha kufua umeme wa gesi cha Kinyerezi II, Mhandisi Ambakisye Mbangula, akiwa kwenye karakana ya kituo hicho leo Januari 9, 2019.
 Meneja wa Kituo cha kufua umeme wa gesi cha Kinyerezi II, Mhandisi Ambakisye Mbangula, akiwa na mwangalizi wa karakana hiyo.
Mhandisi Manda akifafanua jambo kwenye chumba cha udhibiti mitambo (Control room) cha Kituo hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.