Habari za Punde

WAWEKEZAJI WABABAISHAJI KATIKA HIFADHI ZA BAHARI KUONDOLEWA-MPINA


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, katikati wakati wa ziara yake akikagua Eneo Tengefu la Kisiwa cha Mbudya, kushoto Ndg. Msafiri Said Mgoha, ni mmoja wa wasafirishaji wa Wageni kutoka hoteli ya White Sands kwenda Mbudya kulia Kaimu Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Ndg. John Komakoma.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiangalia mmoja ya magofu yanayosadikiwa ni la Shariff, Aliyezikwa katika miaka 500, iliyopita  katika eneo tengefu la Kisiwa cha Mbudya,kulia Mfanyakazi wa Hifadhi hiyo Anita Julius akiwa na Hussein Mwinyogogo ni mlinzi wa kujitolewa katika Kisiwa hicho. 


Na.John Mapepele.

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametoa mwezi mmoja kwa wawekezaji walioingia mikataba ya uwekezaji kwenye Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) kulipa deni la shilingi milioni 331.2 wanalodaiwa vinginevyo Serikali itavunja mikataba na wahusika wote watakamatwa na kutaifishwa mali zao ili kufidia fedha za umma.Waziri Mpina ametoa agizo hilo wakati akizungumza katika ziara ya kutembelea Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu kwenye Visiwa vya Mbudya na Bongoyo ambapo ilibainika kuwa baadhi ya wawekezaji waliopewa maeneo kwenye hifadhi hizo kushindwa kuyaendeleza kwa mujibu wa mikataba sambamba na kushindwa kulipa tozo stahili za Serikali zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.Alisema Serikali ya awamu ya tano haiwezi kukubali kuchezewa na wawekezaji ambao hawajajipanga na kuchelewesha uendelezaji wa fukwe na maeneo mengine ya urithi wa nchi yetu sambamba na kukwamisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Waziri Mpina alisema Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu ina utajiri na urithi mkubwa wa nchi yetu kwa kuwa na fukwe ndefu na nzuri za kipekee duniani, makaburi yenye historia ya kuvutia, mazalia ya samaki, matumbawe yenye mvuto wa kipekee na ndege wa aina za kipekee ambao hawapatikani maeneo mengine duniani. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.