Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa
Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akishiriki ujenzi
wa vyumba vya bweni la Wasichana shule ya Sekondari Kirare Jijini
Tanga mara baada ya kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya zahanati ya
Mapojoni na bweni hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi
kushoto ni Diwani wa Kata hiyo (CCM) Mwagilo anayefurahia ni Mkuu wa
wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Ummy ambaye alikuwa ameambatana na viongozi
mbalimbali wa wilaya ya Tanga akiwemo Mkuu wa wilaya hiyo Thobias
Mwilapwa ambapo alikwenda Kata ya Kirare kuwakabidhi mabati 100 kwa
ajili ya bweni hilo na zahanati ya mapojoni alipofika kwenye eneo hilo
la ujenzi huo alichanganya mchanga na sarauji na baadae kuchapia
ukutani.
Ujenzi huo wa Bweni la Wasichana kwenye shule
hiyo litasaidia kuondosha changamoto ya watoto kutembea umbali wa
kilomita kumi na tano kufuata huduma ya elimu jambo ambalo linaweza
kupelekea kukumbana na vishawishi ambavyo vinaweza kukwamisha ndoto
zao.
Akizungumza mara baada ya kushiriki ujenzi
huo Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa
Tanga alisema atashirikiana na wananchi kuhakikisha changamoto
mbalimbali zinazowakabili zinapatia ufumbuzi.
Alisema kwamba Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchapa kazi
kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kutatua changamoto wa wananchi ili
ziweze kupata ufumbuzi haraka na kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa
maendeleo kwao na jamii zinazowazunguka.
Sambamba na
Waziri huyo kuchangia mabati hayo wakati huo huo Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imeguswa na changamoto hiyo
na kuchangia mabati 50 na saruji 70 katika ujenzi wa bweni la
wasichana la shule ya Sekondari Kirare na kushiriki kwenye shughuli za
ujenzi.
Alisema atahakikisha anashirikiana na wananchi
kwenye maeneo mbalimbali kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto
za Afya ambazo zinaweza kuwa kikwazo kwenye kujiletea
maendeleo.
“Labda niwaambie tu kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais
wetu Dkt John Magufuli imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha changamoto
mbalimbali zinapatiwa ufumbuzi hivyo endeleeni kushirikiana nayo
kuweza kupata mafanikio “Alisema Waziri Ummy.
No comments:
Post a Comment