Habari za Punde

Serikali Kusimamia Maadili ya Askari Polisi

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea salamu baada ya kuwasili katika Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Ulinzi Shirikishi yaliyofanyika Visiwani Zanzibar. Lengo la mafunzo hayo ni kudhibiti uhalifu Visiwani humo
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wahitimu wa Mafunzo ya Ulinzi Shirikishi (hawapo pichani), wakati wa Kufunga mafunzo hayo katika Mkoa wa Kusini Unguja.Lengo la mafunzo hayo ni kudhibiti uhalifu Visiwani Zanzibar
Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Saleh Mohamed Saleh, akizungumza na wahitimu wa Mafunzo ya Ulinzi Shirikishi (hawapo pichani), wakati wa Kufunga mafunzo hayo katika Mkoa wa Kusini Unguja.Lengo la mafunzo hayo ni kudhibiti uhalifu Visiwani Zanzibar.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
Wahitimu wa Mafunzo ya Ulinzi Shirikishi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati akizungumza na kufunga mafunzo ya Ulinzi Shirikishi Visiwani Zanzibar.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Mwandishi Wetu
Serikali imesema haitakua tayari kuona Jeshi la Polisi linachafuliwa na baadhi ya Askari Polisi wasiofuta maadili huku ikisisitiza haitosita kumchukulia hatua askari atakaebanika kukiuka maadili
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akifunga mafunzo kwa Vikundi vya Ulinzi Shirikishi Visiwani Zanzibar ambapo jumla wa walinzi 681 walihitimu mafunzo hayo
Akizungumza na wahitimu pamoja na askari katika hafla hiyo Naibu Waziri Masauni alisema Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na askari polisi waadilifu huku akiweka wazi kuwepo kwa askari wasio waadilifu
“Jeshi letu la Polisi lina miiko yake katika utendaji wa kazi zake,lakini wapo askari wachache wanaovujisha taarifa kwa wahalifu, wanasaidia wahalifu kutenda makosa sambamba na kupokea rushwa,hali hiyo haikubaliki na atakebainika hatutosita kumchukukia hatua kwa mujibu wa taratibu za jeshi,” alisema Masauni
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Saleh Mohamed Saleh, aliwataka wananchi kufichua wahalifu wanaowafahamu katika makazi yao ili matendo ya uhalifu yaweze kupungua
“Polisi Jamii ni dhana pana,tunawategemea wananchi mtusaidie kufichua wahalifu katika maeneo mnayoishi maana uhalifu ukifanyika nyie ndio mnaathirika hivyo basi ni bora mkawa mabalozi wazuri katika maeneo yenu kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi,” alisema Kamishna Saleh
Katika mafunzo hayo jumla ya Walinzi Shirikishi 681 walihitimu ambapo walipitishwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo ukamataji salama,namna ya kuendesha doria,jinsi ya kumfikisha mtuhumiwa kituo cha polisi na elimu jinsi ya kujikinga na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.