Wananchi wakiwa katika usafi wa mazingira katika eneo la kango ya barabara ya Mkapa wakifanya usafi wa mazingira, katika mtaro wa maji kando ya barabara hiyo.
Na.Hafsa Golo.
Umuhimu wa kufanya usafi kuwa jambo muhimu lililohimizwa na vitabu vya dini ili mja alitekeleze bado, limekuwa ni suala zito hasa katika maeneo ya makaazi.Tabia hiyo imekuwa ikirudisha nyuma juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na vyombo vilivyokabidhiwa dhamana ya kusimamia ikiwemo Baraza la Manispaa ya mjini.
Bila ya shaka uzito huo, unakuja pale baadhi ya watu kutokuwa tayari kufuata maelekezo yanayotolewa na chombo hicho ikiwa ni pamoja na utupaji wa taka ovyo uliokithiri baadhi ya maeneo.
Wapo wanaodhani chombo hicho ndicho chenye jukumu pekee la kuweka mazingira safi na kusahau ya kwamba dini inasema usafi ni wajibu wa kila mmoja.Hivi karibuni gazeti hili lilimnukuu Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa ya Mjini, Said Ahmada kwamba mpango mikakati wa awali wa uwekaji wa mji wa Zanzibar safi ulishindikana kutokana na vyanzo mbali mbali ikiwemo ukiukwaji wa sheria sambamba na uhaba wa nyezo.
Hata hivyo, kiongozi huyo hakuridhika na hilo, hatimae aliamua kuandaa mipango mengine ili kuhakikisha wanaweza kufanikiwa ambapo kwa awali alisitisha uwekaji taka katika Mjimkongwe.Mbali na hilo, mikakati mengine iliyobora imeandaliwa kama vile uwekaji wa madebe ya kurupia daka na matangazo maeneo mbali mbali ambayo bila ya shaka yatasaidia kutoa wito kwa jamii.Ikumbukwe utalii Zanzibar unachangia asilimia 27 za pato la taifa hivyo ipo haja ya kuweka mji wetu safi kwani ndio roho na kiini cha uchumi wa taifa.
Kwa upande mwengine ni jambo la aibu nchi kama Zanzibar, kusikia imefeli kiusafi hasa ikizingatiwa ni miongoni mwa visiwa vyenye historia nzuri katika mataifa mengine duniani.
Isitoshe wapo baadhi ya wananchi hapa nchini husikika wakisifia mji wa Arusha kwa usafi sambamba na kuponda visiwani mwao bila ya kutafakari au kujiuliza kwanini wao waliweza na vipi sisi tushindwe?
Nafikiri si wakati wa kuonesheana vidole jambo la msingi tushikamane sote kwa pamoja kuweka mji wetu safi kwani “kidole kimoja hakivunji chawa”.

No comments:
Post a Comment