Wataalamu wa Tanesco ,REA na Mkandarasi wakipokea maagizo kutoka kwa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani
Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano huo leo. |
WACHIMBAJI
wadogo mkoani Geita wanatarajiwa kufikishiwa Umeme katika mashimo yao ili
kuwawezesha kufanya shughuli zao za uchimbaji kwa ufanisi mkubwa.
Hayo
yalisemwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani wakati akizungumza katika
mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Imwelu kilichopo wilaya ya Chato mkoani
Geita.
Alisema
kuwa Serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika maendeleo ya nchi
na kwa sasa umeme utafikishwa katika mashimo ya wachimbaji ili kurahisisha
shughuli zao za uchimbaji.
“Ndugu
zangu wachimbaji tumeshaanza kuwapa transfoma kwa hiyo kama wewe ni mchimbaji na
unataka uchimbaji wao uwe wa kisasa,utajaza fomu itakayowezesha kuendesha
mashine zenu za kuchakata madini”Alisema.
Waziri
huyo aliwasihi wachimbaji wadogo kutumia fursa ya umeme ili kuleta tija katika
uchumbaji wao na hivyo kuweza kuongeza pia ufanisi mkubwa.
Hata
hivyo Waziri Kalemani alimtaka Mkandarasi na Tanesco kufikisha umeme katika
kijiji hicho ndani ya siku ishirini (20)
No comments:
Post a Comment