Habari za Punde

Apelekwa Rumande kwa tuhuma za wizi na pia kupatikana na mali inayodhaniwa kuwa ya wizi

Na Masanja Mabula –Pemba.

MAHAKAMA ya wilaya Wete imempeleka rumande kwa  muda wa  siku kumi na mbili mtuhumiwa Juma Haji Juma  23 mkaazi wa mchangamdogo baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Mtuhumiwa huyo   amefikishwa mahakamani hapo akiwa na mwenzake Ali Omar Massoud 34 wa Mchangamdogo  ambaye yeye yuko nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa mwili tofauti , moja la wizi na kosa la pili ni kupatikana na mali inayodhaniwa kuwa ya wizi.

Imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka wa serikali Juma Mussa ,mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Deo k Kalimi kwamba siku ya tarehe 27/11/2018, wakati usiofahamika , huko Kambini , Juma Haji Juma aliimba mchele polo 3 zikiwa na thamani ya 250,000/= kwa makisio mali ya Ali Hamad.

Aidha tarehe 29/11/2018, saa tatu asubuhi huko chwale madenjani mtuhumiwa Ali Omar Massoud , alipatikana na polo moja ya mchele yenye uzito wa kilo 50 ambao unadhaniwa kuwa ni mali ya wizi.

Watuhumiwa hao wametakiwa kuwa na wadhamini wawili madhubuti pamoja na vitambulisho halisi na barua ya sheha , masharti ambayo yamemshinda Mtuhumiwa Juma Haji Juma huku mwenzake akipeta baada ya kutimiza masharti hayo.
Kesi yao imepangwa kuendelea tena tarehe 12 Machi mwaka huu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.