Habari za Punde

Masheha wateule waapishwa Wilaya ya Chake

 MASHEHA wateuliwa Hamad Abdalla Ali wa shehia ya Msingini na Mbwana Ali omar wa Ngambwa Wilaya ya Chake Chake, wakisubiri muda kufika ili kula kiapo cha uteuzi wa kuwa shehai wa shehia zao, hafla iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 SHEHA  wa shehia ya Msingini Wilaya ya Chake Chake Hamad Abdalla Ali, akila kiapo cha kuteuliwa kuwa sheha wa shehia hiyo, huku viongozi mbali mbali wa serikali na kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kusini Pemba, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Hemed Suleiman Abdalla.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akimuangalia sheha wa shehia ya Msingini Hamad Abdalla Ali, wakati alipokuwa akila kiapo cha kuwa sheha wa shehia hiyo, halfa hiyo iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa Chake Chake Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

SHEHA wa Shehia ya Ngambwa Wilaya ya Chake Chake Mbwana Ali Omar, akila kiapo cha kuteuliwa kuwa sheha wa shehia hiyo, Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa Chake Chake Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.