Habari za Punde

Ufungaji wa Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.

 Mkuu wa Idara ya Maradhi ya Kina mama na Uzazi Hospitali ya Mnazi Mmoja Dkt,Ummulkulthum Omar akiwasilisha mada kuhusu Uzazi katika ufungaji wa  Mkutano wa 11 wakutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
 Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Afya waliohudhuria katika ufungaji wa  Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
 -Mkurugenzi Utawala na Uendeshaji Hospitali ya Mnazi Mmoja Abubakar Khamis Hamad akiuliza maswali katika mkutano wa 11 wakutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
 Daktari Bingwa wa maradhi ya akina mama Hospitali ya Mnazi mmoja Hamed Mahfudh akifafanua baadhi ya maswali yalioulizwa katika ufungaji wa  Mkutano wa 11 wakutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdulla akitoa hotuba ya ufungaji wa Mkutano wa 11 wakutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 01. 03.2019
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ zitaendelea kujenga Nyumba za kuishi Wahudumu wa afya katika kila eneo lenye Kituo cha Afya ili kuhakikisha wahudumu hao wanapatikana muda wote hasa maeneo ya Vijijini.
Kwa kufanya hivyo kutapunguza kasi ya wahudumu hao kukimbilia kufanyakazi Mijini na kuviacha vituo vya Afya vya Vijijini bila wahudumu.
Hayo yameelezwa katika Mkutano wa 11 wa kutathmini maendeleo ya sekta ya Afya kwa mwaka 2017/2018 ikiwa ni mapendekezo yaliyotolewa na washiriki wa mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa Hotel ya VERDE, nje kidogo ya mjini Zanzibar.
Katibu wa Wizara ya Afya Asha Ali Abdulla amesema mkutano huo umekuwa wa mafanikio makubwa kutokana na kujadili mambo muhimu na mapendekezo ya kuimarisha huduma ya afya kwa mwaka 2019/2020.
Amesema katika kukabiliana na changamoto ya maradhi yasiyoambukiza ikiwemo Maradhi ya Miguu, Mgongo ambayo yamekuwa yakiwasumbua wananchi wengi wa Zanzibar Katibu huo amesema mkutano umependekeza kufanya tafiti mbali mbali kubaini chanzo cha maradhi hayo.
Hata hivyo amesisitiza kutolewa kwa elimu ya afya kuhusu maradhi mbali mbali kama vile Shinikizo la Damu, Kisukari na Saratani ili wananchi waweze kubadili mifumo yao ya maisha ambayo huchangia ongezeko la maradhi hayo.
Amesema njia muhimu ni kuhakikisha wananchi wanakula vyakula salama na kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuiepusha miili yao na kitisho cha maradhi hayo.
Kwa upande wake Atie Juma Shaame Mkurugenzi wa Mipango sera na utafiti Wizara ya Afya amesema licha ya huduma kutolewa bure Serikali itaendelea kuimarisha huduma hiyo kwa kiwango cha juu kabisa.
Amesema kwa upande wa Serikali kupitia Wizara ya Fedha imeahidia kushirikiana na Wizara hiyo pamoja na washirika wa maendeleo ili kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi Zanzibar Amina Abdulqadir amesema mkutano huo umekuwa na mafanikio makubwa hasa kutokana na kushirikisha wadau wote kutoka Serikalini na Taasisi binafsi ambao michango yao ilikuwa muhimu.
Amesema Sera ya ugatuzi itasaidia kwa kiasi kikubwa kupatikana wauguzi watakaokidhi haja ya kila eneo na kusisitiza serikali kutoa elimu kwa wananchi kufahamu maana halisi ya ugatuzi.
"Ugatuzi kwa kweli umesaidia sana kupeleka madaraka mikoani kubwa linalohitajika ni kuhakikisha kuwa Wananchi wanapatiwa elimu wajue hasa maana ya Ugatuzi ili waweze kutoa ushirikiano ipasavyo" alisema Mwenyekiti Amina
Amesema akiwa Mwenyekiti wa Wauguzi jukumu lake ni pamoja na kuwakumbusha wenzake kutumia lugha nzuri wakati wanapowahudumia wagonjwa.
kila inapofika kipindi cha uandaaji wa Bajeti mpya Wizara ya Afya huwaita wadau wake wote kujadili namna ya kuimarisha sketa hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Kwa takriban miaka 15 sasa Wizara ya afya imekuwa ikifanya mikutano ya kutathmini matokeo ya utekelezaji wa kipindi cha mwaka mmoja ambapo mwaka huu mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na washiriki zaidi ya 120 kutoka sekta binafsi, Washirika wa maendeleo wakiwemo WHO, UNICEF, UNFPA, UNDP, ujumbe wa mwaka huu ‘‘Kuimarisha ushikiriano kwa lengo la kuinua huduma za Afya bora kwa wote ’’

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.