Habari za Punde

Wananchi wa Majimbo wa Fuoni na Pangawe Wapata Skuli Mpya ya Msingi na Maandalizi ya Kisasa Yazinduliwa leo.

Jengo la Ghorafa Mbili la Skuli ya Msingi na Maandalizi Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi "B"Unguja iliofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika eneo la Fuoni Mambosasa. lililojengwa kwa Msaada kutoka Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukamilisha ujenzi huo.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma, alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi "B" Unguja kwa ajili ya Ufunguzi wa Skuli hiyo.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwakilishi wa Balozi Mdogo wa China ZanzibarBi. Shen Qi, alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi na Maandalizi Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi"B"Unguja.katika hafla ya ufunguzi wa Skuli hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisoma Jiwe la Msingi la Skuli ya Fuoni Pangawe baada ya kuweka Jiwe la Msingi na Kuifungua Skuli hiyo kulia Mwakilishi wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar.Bi. Shen Qi, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vyac Skuli hiyo Fuoni Mambosasa leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata Utepe kuashiria Uzinduzi wa Skuli ya Maandalizi na Msingi ya Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi "B"Unguja kushoto Waziri wa Eilimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na Mwakilishi wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Bi. Shen Qi na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,Mhe. Haji Omar Kheri na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakishuhudia Uzinduzi huo uliofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika moja ya madfarasa ya Skuli hiyo baada ya kuifungua leo, akiwasalimia Wanafunzi waliokuwemo katika darasa hilo wakati Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Idrissa Muslim Hijja akitowa maelezo kwa Rais. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dl. Ali Mohamed Shein, akitembelea chumba cha Maktaba ya Skuli hiyo baada ya ufunguzi wake, kulia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali ZXanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na kushoto Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo yta Amali Zanzibar Dkt. Ifrissa Muslim Hijja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Mhe, Haji Omar Kheri.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika chumba cha maabara ya sayansi ya skuli hiyo baada ya kuifungua rasmin leo. 
Katibu Mkuu wa Wuizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Idrissa Muslim Hijja akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, alipotembelea chumba cha Maktaba ya Skuli hiyo ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe baada ya kuifugua rasmin leo. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akitembelea jengo la Skuli ya Msingi na Maandalizi la Fuoni Pongwe, akimsikiliza Waziri wac Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na kushoto Katibu Mkuu Wizara Elimu na Mafunzo ya Amali Dkt.Idrissa Muslim Hijja. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.