Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Afunguac Skuli ya Msingi na Maandalizi Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi"B" Unguja leo 23-/3/2019.

Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Pangawe Wilaya ya Magharibi "B" Unguja kushoto Khalid Khamis na kulia Mudrik Said wakisoma Qurani na Tafsiri yake wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi "B"Unguja iliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein. 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Idrissa Muslim Hijja akitowa maelezo ya kitaalam yac ujenzi wa Majengo ya Skuli ya Msingi na Maandalizi Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi "B"Unguja wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi uliofanyika leo.
Mwakilishi wa Balozo Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China Zanzibar.Bi. Shen Qi, akitowa salamu za Nchi yake wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe iliojengwa kwa msaada kupitia Serikali ya China.kwa kushirkiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Waziri wa cEilimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma akizungumza wakatin wa hafla hiyo ya Ufunguzi wa Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi"B" Unguja kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuzungumza na Wananchi katika hala hiyo leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi"B" Unguja iliojengwa kwa msaada na Serikali ya Watu wa China kwa kushiurikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. kulia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na Mwakilishi wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar.Bi. Shen Qi. 
Wanafunzi wa Skili ya Msingi ya Fuoni na Pangawe wakiwa katika hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika viwanja vya Skuli hiyo Fuoni Mambosasa leo.
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Skuli ya Maandalizi na Msingi katika viwanja vya Skuli hiyo Fuoni Mambosasa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wac Baraza la Mapinduz Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.