Habari za Punde

Hafla ya uzinduzi wa kikundi chja akinamama cha Green Rose jimbo la Kiembesamaki

 Mjumbe wa NEC Amini Salmin Amour akitoa nasaha zake kwa kinamama wa kikundi cha Green Rose kiliopo Jimbo la Kiembesamaki katika hafla ya uzinduzi wa kikundi hicho uliofanyika Tawi la CCM Mchina Mjini Unguja.
 Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Ibrahim Raza akizungumza na Kinamama wa Kikundi cha Green Rose mara baada ya kukizindua kikundi hicho kinachojishuhulisha na utengenezaji wa Mabatiki na Sabuni za aina mbalimbali katika hafla iliyofanyika Tawi la CCM kwa Mchina.
  Wakinamama wa Kikundi cha Green Rose (UWT) Jimbo la Kiembesamaki wakimsikiliza Mbunge wao (hayupo pichani) Ibrahi Raza alipokuwa akizungumza nao.
 Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Raza (katikati) akiwa na wanakikundi cha Green Rose katika picha ya pamoja. Kushoto ya Mjumbe wa NEC Amini Salmin Amour.
Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.