Baadhi
ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia
kiwango cha asilimia 95.
Mkurugenzi
wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Bw, Paul Rwegwasha
akitoa taarifa fupi ya Mamlaka kuhusu mpango wa
usimamizi na uendeshaji jengo la III la abiria kwa Kamati ya kudumu ya
Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo mapema leo.
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu
ambaye ni Mbunge wa Kasulu mjini Mhe, Daniel Nsanzugwako (mwenye kofia)
akiuliza swali mara baada ya kusomwa taarifa ya mradi wa Jengo la III la abiria
wakati Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua
maendeleo ya mradi huo mapema leo.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa
(Mb) akijibu hoja maswali mbalimbali ya kisera kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Jengo la III la abiria
mapema.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi
Atashasta Nditiye alipokuwa akijibu maswali kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea
kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la III la abiria mapema leo aliekaa kushoto ni Mwenyekiti wa
Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Mpanda Vijijini Moshi Selemani Kakoso.
Mhandisi
Burton Komba kutoka Wakala wa Barabara akitoa maelezo ya Ujenzi wa Jengo la III
la abiria kwa Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipofanya ziara katika Jengo hilo
mapema leo.
MAMLAKA
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imebainisha kwamba itakua tayari kwa ajili
ya utoaji wa huduma za uendeshaji katika Jengo la tatu la abiria pale mradi wa
Ujenzi utakapokuwa umekamilika.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha alipokua akitoa taarifa
fupi ya TAA kwa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu ilipofanya ziara
katika eneo la Ujenzi huo.
Bw.
Rwegasha amesema hatua mbalimbali za Maandalizi tayari zimeshachukuliwa kwa kushirikiana
na wadau wa huduma hizo, ikiwa ni pamoja na utoaji wa mafunzo yanayohitajika
kwa watendaji wa ngazi mbalimbali.
“Mamlaka
inaendelea kufanya taratibu za maandalizi
ya utoaji huduma za uendeshaji katika Jengo la tatu la abiria, katika mpango
huo tayari mafunzo kwa watendaji mbalimbali yameanza na hivi sasa watendaji 40
wapo Korea ya kusini katika mafunzo” amesema Bw. Rwegasha.
Aidha
Bw. Rwegasha amebainisha kwamba katika utekelezaji mpango wa uhamishaji
shughuli, Mamlaka imejipanga kuhakikisha hakuna madhara yeyote ya kiuendeshaji
yanajitokeza.
“Mamlaka
itahakikisha kwamba inazuia athari zote zinazoweza kutokana na zoezi la
uhamishaji wa shughuli za uendeshaji ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa Ndege na
abiria, uharibifu wa mitambo,madhara ya kiusalama na kadhalika.
Katika
hatua nyingine, Mkurugenzi wa Idara ya Viwanja vya Ndege katika Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Emmanuel Raphael amebainisha kwamba hadi kufika mwezi February
2019 utekelezaji wa kazi zote ulifikia asilimia 95.
“Ujenzi
wa kazi zote za Ujenzi umefikia 95%, ambapo mchanganuo unaonesha kwamba ujenzi
wa jengo umefikia 96%, maegesho ya magari 92%, maegesho ya ndege 98% na kwa
ujumla kazi zinaenda vizuri na zinatarajiwa kukamilika Mei 31, 2019”, alisema
Mhandisi Raphael.
Naye,
Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
amebainisha kwamba mpaka sasa Wananchi wa Kipawa waliopisha upanuzi wa Kiwanja
wameshalipwa fidia na kwamba mpaka sasa hamna mgogoro wa fidia.
Akitoa
majumuisho baada ya ziara ya kamati katika eneo la ujenzi, Mwenyekiti wa Kamati
hiyo ya Bunge, Mhe. Seleman Kakoso amesema kwa ujumla Kamati imeridhishwa na
hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kwamba wameridhishwa na namna pesa ya serikali
ilivyotumika.
“Kwa
ujumla Kamati imeridhishwa na hatua ya Ujenzi iliyofikiwa, matumizi ya pesa ya
Serikali yanaonekana ni mazuri, lakini natoa wito kwa TAA kuongeza kasi ya
maandalizi ili kwenda sawa na kasi ya ujezi huu, lakini pia mjipange kuongeza
wafanyakazi ili kuhakikisha kwamba watendaji wa huduma za uendeshaji
wanajitosheleza”, amesema Mhe. Kakoso.
No comments:
Post a Comment