Habari za Punde

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Akifungua Mkutano wa Kuzungumzia Udhalilisahaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Mwanajuma Majid Abdulla akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) kujadili uzallishaji uliokithiri hapa Zanzibar hafla hiyoimefanyika  ukumbi wa Wizara hiyo Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.(Picha na Mwashungi Tahir wa Habari Maelezo.

Na Mwashungi    Tahir    Maelezo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi  Uwezeshaji, Wazee Wanawake na Watoto Mwanajuma Majid Abdullah aliwataka waandishi wa habari kutoa  elimu  zaidi kwa jamii kuhusu vitendo vya udhalilishaji vinavyozidi kuongezeka kwa wanawake na watoto nchini.
Hayo ameyasema huko katika ukumbi wa wizara  wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa kuhusiana na udhalilishaji wa kijinsia na kutaka njia gani itumike  ili jamii ielewe.
Amesema udhalilishaji wa wanawake na watoto bado unaendelea kila leo matukio ya kuhuzunisha yanaendelea  na kuwataka wazazi na walezi kuwa nao watoto wao karibu ili kuzijua nyendo zao za kila siku.
Aidha alisema hivi sasa udhlilishaji uko wa aina nyingi ukiwemo ubakaji, utoroshaji wa watoto wanapokuwa wanatoka skuli au madrasa  na pia kudungwa sindano na watu wasiojulikana na kuzikwa vitoto vichanga.
Hivyo amewaomba waandishi wa habari kuwa na mashirikiano na Wizara katika kuhakikisha suala hili linamalizika kabisa kwa jamii kupatiwa elimu zaidi juu ya vitendo hivi.
Pia amewaonya wazazi kupeana talaka ovyo kwani jambo hili linaleta mfarakano wa watoto na kukosa malezi mazuri na hatimae kudhalilishwa kwa kuwa ombaomba.
Nae Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Mghaza Gharib Juma amewataka waandishi wa habari kusaidiana juu ya vitendo vya udhalilishaji  na kupanga mikakati kwa kuielimisha jamii .
Vile vile  tuimarishe malezi juu watoto kwa kuwatunza na kuwaweka karibu nao ili wanapotokewa na tatizo wawe wazi kusema linalowatokea,  wafahamishwe matukio yanayotokea ya udhalilishaji ili likiwatokea wawe tayari washapewa taarifa.
Kwa upande wa waandishi wa habari kutoa michango ili suala hili liweze kufikia hatua nzuri wamesema malezi ya zamani yarudi kwani mtoto wa mwenzio nae wako , pia matukio ya wanaofanya vitendo hivyo yatolewe hukumu  mara moja na kuwataka jamii ijitokeze kutoa ushahidi na kuacha muhali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.