Habari za Punde

ZUPHE Wametakiwa Kushirikiana Ili Waweze Kujenga Nguvu ya Pamoja Kutatua Matatizo Sehemu za Kazi.

Na.Takdir Suweid.
Viongozi wa Matawi na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Chama cha wafanyakazi wa huduma za jamii na Afya Zanzibar (ZUPHE) wametakiwa kushirikiana ili waweze kujenga nguvu ya pamoja katika kutatua matatizo yanayowakabili sehemu za kazi.
Amesema miongoni mwa kazi za wafanya kazi ni kutetea maslahi nya wafanyakazi,kutoa elimu na kuwawakilisha wafanyakazi katika maeneo ya utetezi ili waweze kupata haki zao za msiongi hivyo iwapo watashirikiana wataweza kupata haki zao na kufikia malengo yaliokusudiwa.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanya kazi Zanzibar (ZATUC) Khamis Mwinyi Muhammed alipokuwa akifunguwa  Mafunzo elekezi kwa Viongozi hao,Mafunzo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa akili Kidongochekundu.
Amesema kazi za msingi ya vyama vya wafanyakazi ni kutatua migogoro katika sehemu za kazi sio kuwaachia wanachama pekee.
Aidha ameupongeza uongozi wa Zuphe Taifa kwa kuweka mikakati madhubuti ilioweza kukifanya chama hicho kuwa imara na kuweza kutetea maslahi ya wananchi wake.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa Zuphe Taifa Bi Jina Hassan Silima amesema mafanikio yaliopatikana yanatokana na juhudi na mashirikiano yaliopo baina ya Viongozi na Wanachama wanaowaongaza.
Miongoni mwa mada zilizowasilishwa katika Mafunzo hayo elekezi ya siku moja ni pamoja na Historia ya vyama vya wafanyakazi na Majukumu ya Viongozi wa matawi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.