MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati uzinduzi wa mradi wa afya kamilifu wa huduma na matibabu ya kufubaza virus vya Ukimwi katika mikoa ya Tanga na Zanzibar. |
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa uzinduzi huo |
Mkurungenzi Mkazi wa Amref Health Afrika Dkt Florence Temu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo |
MENEJA wa mradi wa Afya kamilifu Dkt Edwin kilimba akizungumza wakati wa uzinduzi huo |
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizundua mradi huo |
Sehemu wa washiriki wakifuatilia uzinduzi huo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Amrefu kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia ni Mkurungenzi Mkazi wa Amref Afrika Dkt Florence Temu
Picha ya pamoja
SHIRIKA la Amref Health Afrika leo limezindua mradi wa Afya Kamilifu wa huduma na matibabu ya kufubaza Virusi vya Ukimwi katika mkoa wa Tanga na Visiwani Zanzibar utakaokuwa wa miaka mitano
Akizungumza wakati akizundua mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliwataka viongozi wa mkoani humo wametakiwa kuhamasisha waumini wao kuona umuhimu wa kupima kwa hiari afya zao ikiwemo kuacha tabia ya kuwanyanyapaa waathirika wa UKIMWI walioko katika jamii.
Alisema kuwa
viongozi hao wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanawasaidi waumini wao kuona
umuhimu wa kutambua afya zao na wale walioathirika wajitambue na kuwa tayari
kuanza matibabu ya dawa .
“Licha ya mkoa
wa Tanga kiwango cha maambukizi kufikia
asilimia 5% inahitajika nguvu ya ziada katika kuhakikisha tunapunguza kasi ya
maambukizi mpya kwa kuanza kufanyia utafiti maeneo ambayo ni visababishi vya
ugonjwa huo”alisema Mkuu wa mkoa huyo.
Alisema kuwa
kwani tafiti zinaonyesha kuwa nchini Tanzania kuna watu takribani mil 1,4 ambao
wanaishi na VVU lakini wanaotumia dawa za kufubaza ugonjwa huo ni wachache sana
hivyo lengo la serikali ni kuwatambua wao hao na kuhakikisha wanatumia dawa ili
kupunguza kasi ya maambukizi mpya.
Kwa upande
wake Mkurungenzi Mkazi wa Amref Health Afrika Dkt Florence Temu
alisema kuwa mradi
wa afya kamilifu unalenga katika kuongeza idadi ya watu wanaojijua kuwa
wanaishi na VVU na UKIMWI wanaopata huduma za matibabu ya kufubaza virus hivyo
ili kuhakikisha vinafubazwa.
Alisema kuwa
wamelenga katika kuhakikisha kwamba katika kipindi cha miaka mitano ya
utekelezaji wa mradi huo watu wote wanaoishi na VVU na UKIMWI wanaishi mkoani
Tanga kujua hali zao na kupata matibabu kamilifu.
“Katika
kipindi cha miezi sita ya utekelezaji wa mradi huo tumeweza kubaini kesi za
waathirika wa UKIMWI zaidi 3000 ,na wameweza kuanzishiwa matibabu ya dawa za
kufubaza ugonjwa huo mara baada ya kubaini kuwa wameathirika”alisema
Dkt Temu.
Hata hivyo
Meneja wa mradi wa Afya kamilifu Dkt Edwin kilimba alisema kuwa
mradi huo
utaimarisha ufuatiliaji na tathimini kiasi cha kupata taarifa halisi za
maendeleo katika muda halisi ili kuimarisha usimamizi bora
“Mradi
unaunga mkono malengo mapya ya progamu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa kuhusu VVU
/UKIMWI kwa kupanua tiba ya kufubaza virusi ili kumaliza janga la ugonjwa huo
hapa nchini ifikapo mwaka 2030”alisema Dkt Kilimba.
Vile vile
alisema kuwa mradi huo utaweza kuimarisha mifumo ya afya kwa watu wanaoishi na
UKIMWI kwa ajili ya kuwapatia huduma za matunzo na tiba katika vituo vya afya
ili kuweza kufanyakazi kwa ufanisi hasa katika wilaya ambazo mradi huo
unafika.
No comments:
Post a Comment