Habari za Punde

Mabingwa wa ligi Kuu Zanzibar KMKM wakabidhiwa rasmi kombe lao

Na Hawa Ally
MABINGWA wapya wa ligi kuu ya Zanzibar KMKM wamekabidhiwa kombe lao jana rasmi baada ya kukamilisha mechi yao ya mwisho Kati yao na JKU.


KMKM wamefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kufikisha  pointi 80 ubingwa ambao walioukosa karibu miaka mitano .

Kombe hilo walikabidhiwa na kamishna wa Michezo Sharifa Khamis  ambae alikuwa mgeni rasmi wa mchezo huo wa kumalizika ratiba kwa timu zote.

Katika mchezo huo KMKM walianza kuandika bao la Kwanza mnamo dakika ya 34 kupitia kwa mfungaji wake Mussa Ali Mbarouk ambalo lilidumu Hadi  mapumziko.

KMKM ambao walitangulia kupata ubingwa.huo wakiwa na mchezo mmoja mkononi waliingia kipindi cha pili na kuendelea kuliandama lango la wapinzani wao hao .

Bao la pili la KMKM lilifungwa tena na Mussa Ali Mbarouk ambae amefikisha bao la 23 na kutangazwa kuwa mfungaji Bora na Abuubakar Khamis Sufiani wa zimamoto ambae nae alifunga idadi Kama hiyo lakini alitangazwa kuwa mchezaji Bora.

 Mapema uwanjani hapo kulikuwa na mchezo Kati ya Zimamoto na Polisi ambapo ulimalizika kwa Zimamoto kushinda mabao 2-1.


Katika mchezo huo Zimamoto mabao yake yalifungwa na Abuubakar Khamis Sufiani na Mohammad Prince na la Polisi likifungwa na Hassan Makame.

Huko katika uwanja wa Mao Ze Dong timu ya Malindi ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mafunzo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.