Habari za Punde

Mwakilishi jimbo la Welezo awaasa wananchi kutochanganya masuala ya siasa na maendeleo


Wilaya ya Magharibi B.            

Wakaazi wa Michikichini na Muembemchomeke wametakiwa kuacha kuchanganya masuala ya siasa na maendeleo.

Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Welezo Hassan Khamis Hafidhi wakati alipokuwa akizungumza na Wakaazi hao mara baada ya kumaliza zoezi la ujenzi wa Daraja la Mtobarafu Wilaya ya Magharibi A.

Amesema maendeleo ya shehia hizo yataletwa na wanashehia wenyewe hivyo hakuna budi kushirikiana katika kuleta maendeleo katika Shehia zao.

Amefahamisha kuwa lengo la kujenga Daraja hilo ni kuwaondoshea usumbufu wanaoupata kwa muda mrefu wakaazi wa eneo hilo kwani imesababisha Madereva wa Daladala kuondosha Gari zao.

Mh. Hassan ambae pia ni Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda ameipongeza Kamati ya maendeleo Sehia ya Mchikichikini kwa kuwa mstari wa mbele kubuni mikakati inayoweza kuwatulia matatizo yanayowakabili  za kushirikiana katika kuleta maendeleo.

Mapema akitoa maelezo katika ujenzi huo Fundi Mkuu wa Daraja hilo Mkubwa Mohammed Omar  amesema ujenzi wa Daraja hilo umejengwa kutokana na nguvu za Wananchi na Viongozi wa Jimbo la Linatarajia kugharimu zaidi ya sh.milioni 35 hadi kukamilika na kuwaomba wafadhili kujitokeza kutoa michango yao kama vile Kifusi na Mifuko ya Saruji.

Nao baadhi ya Wakaazi wa shehia ya Michikichini na Muembemchomeke wasema kukamilika kwa Daraja hilo kutawaondoshea usumbufu mkubwa wanaoupata hasa watoto wao wanapokwenda au kurudi kusoma skuli na chuoni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.