Habari za Punde

SERIKALI HAIJAZUIA BIASHARA YA MADUKA YA KUBADILISHIA FEDHA ZA KIGENI

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu Ukaguzi wa Maduka ya kubadilisha Fedha za Kigeni ambapo alisema lengo lake sio kufuta biashara ya maduka hayo bali ni kudhibiti ukiukwaji washeria uliokithiri na utakasishaji wa Fedha haramu.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, akieleza kuwa jumla ya maduka 87 yamefanyiwa ukaguzi Jijini Dar es Salaam na ni maduka matano pekee ndio yamebainika kutokiuka sheria, wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akifafanua jambo wakati wa mkutano kati yake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu na Kamishna wa Sera wa Wizara hiyo Bw. Mgonya Benedicto .
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi, Sharon Sauwa, akiuliza swali kuhusu kufungwa kwa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni wakati wa Mkutano kati ya waandishi wa habari na  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani) kuhusu ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Waandishi wa Habari na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja (kushoto), wakiwa katika Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), ambapo Waziri huyo alisema hakuna mmliki wa Duka la Kubadilisha Fedha ambaye amewasilisha malalamiko yoyote kwa mamlaka husika kuhusu zoezi la ukaguzi wa maduka hayo.
(Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.