Rais wa Timu ya Villa Uniteds Abdulrabi Mahfoudh (Manji)akizungumza na waandishi wa habari za Michezo kuhusiana na kujitowa kwa Timu yake katika Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Unguja,akizungumza katika ukumbi waKlabu yao Mwanakwerekwe Unguja leo.
Na. Hawa Ally, Zanzibar.
UONGOZI wa timu ya Villa Uniteds “Mpira Pesa “umeamua kuivunja na kuifuta timu hiyo iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza Kanda ya Unguja kwa kuwatuhumu baadhi ya waamuzi na viongozi wa ZFF kuifanyia hujuma timu hiyo.
Akizungunmza na Waandishi wa habari Rais wa timu hiyo Abdurabi Dau “Manji” alisema baadhi ya waamuzi wanashindwa kuzitumia sheria 17 za mpira kama zilivyo badala yake wamekuwa wakifanya upendeleo kwa baadhi yatimu.
Alisema baadhi ya waamuzi wamekuwa wakifungisha magoli ambayo unaona kabisa sio magoli halali nah ii inatokana na mambo mawili aidha vitendo vya rushwa pamoja na kufanya upendeleo kwa timu hususani zile za vikosi.
Aidha alisema walishapeleka malalamiko yao katika chama cha soka Zanzibar ambacho sasa ni shirikisho lakini hakuna jitihada ambazo zilizowezwa kuchukuliwa badala yake timu hiyo inaendelea kuhujumiwa jambo ambalo wachezaji na hata viongozi hawaliridhiki nalo.
Alisema maaamuzi ya kuivunja timu hiyo hayakuwa ya viongozi tu bali hata wachezaji waliokuwa wakiitumikia timu hiyo walichoshwa na vitendo hivyo ambavyo vinasababisha hata kurejesha nyuma jitihada zao za kuona kama soka ni ajira kama zilivyo ajira nyingine.
“Mpira unauma husususani pale unaoona umeonewa hasa , maana tunatumia pesa nyingi kwa kuhidumia tumu, kusajili wachezaji alafu ukija kukuta mambo hayayunayofanyiwa ya kufungishwa kwa makusudi kwakweli jambo hili tumechoka kulivumilia.”Alisema.
Aidha alisema wachezaji wawili waliwasajili kutokea Tanzania bara ambao ni Shabani Abdalla na Mohmed Abdul wanafanya utaratibu wa kuwarejesha kwao ili wakajiendeleze zaidi na soka kwani viwango vyao ni vyakuridhisha.
Rais huyo wa Vila United alisema kuwa anatarajia kuwasilisha barua kwa shirikisho la soka ZFF na kwa mrajisi juu ya kuifuta na kuivunja timu hiyo na haitakuwepo tena.
Timu hiyo ya Villa United hadi inavunjwa ilikuwa imebakisha mchezo mmoja wa kumaliza msimu na ilikuwa katika nafasi ya 3 na alama 57 katika msimamo wa ligi daraja la Kwanza Kanda ya Unguja.
No comments:
Post a Comment