Habari za Punde

Dk.Shein Aipongeza Wizara Hiyo Kwa Kushirikiana Katika Utendaji wa Kazi Zao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Utumishi wa Umma Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman, akiwasilisha ripoti ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yake kwa kipindi cha mwezi Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar 
Rais Dk. Shein amekutana na uongozi wa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo Ofisi hiyo ilieleza kuwa inatekeleza majukumu yake ya msingi kupitia maeneo mawili makuu ambayo ni Usimamizi wa Utumishi wa Umma na Usimamizi wa Utawala Bora.
Akisoma muhtasari wa taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Ofisi hiyo Waziri wa Ofisi hiyo Haroun Ali Suleiman alisema kuwa katika kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019 Ofisi hiyo ilitekeleza mambo  mbali mbali ya kujivunia ikiwa ni sehemu ya majuku yake ya msingi.

Aliongeza kuwa kwa upande wa maendeleo, Ofisi hiyo ilipanga kutekeleza Miradi miwili ya maendeleo ambayo ni Mradi wa Serikali Mtandao na Mradi wa ujenzi wa Jengo la Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar.

Nae Dk. Shein kwa upande wake aliipongeza Ofisi hiyo na kueleza jinsi alivyoridhishwa na maandalizi ya ripoti hiyo Mpango kazi wa miezi tisa.

Dk. Shein alisisitiza haja kwa uongozi wa Ofisi hiyo kwa vile ni ya wafanyakazi alieleza kuwa ni vyema ikawa inawasikiliza wafanyakazi sambamba na kuwatatulia changamoto walizonazo kwani hiyo ni moja wapo ya sifa ya utawala bora.

Aliwataka wafanyakazi wa Ofisi hiyo kushirikiana, kupendana na kuwa kitu kimoja huku wakaizingatia maadili na uzalendo huku wakihakikisha wafanyakazi wanafanya kazi katika mazingira mazuri

Dk. Shein amemaliza vikao vya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Wizara zote za Serikaki ya Mapinduzi ya Zanzibar vilivyoanza Mei 13 mwaka huu katika ukumbi wa Ikulu ndogo Kibweni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.