Habari za Punde

RITTA KABATI CHALLENGE CUP MSIMU WA TATU YAANZA RASMI

Mwenyekiti wa mashindano ya Ritta Kabati challenge cup 2019 Gerald Malekela akizungumza na waandishi wa habari wa mkoani Iringa juu zoezi la uchukuaji wa fomu za mashindano hayo.
Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo msimu wa pili wa mwaka 2018 /2019 (Picha kutoka maktaba)
Kamati anzilishi ya mashindano ya Ritta Kabati Challenge Cup toka msimu wa kwanza mwaka 2017 (picha kutoka maktaba)

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Kamati ya ya mshindano ya Ritta Kabati challenge cup 2019 imezindua rasmi kwa kuanza kuzialika timu kwa ajiri ya kuchukua fomu kushiriki na wameweka bayana jinsi mfumo wa mashindano utakavyokuwa pamoja na zawadi kwa washindi wote. 

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa mashindano hayo Gerald Malekela alisema msimu wa tatu wa mashindano Makubwa kwa ukanda huu wa nyanda za juu kusini ya Iringa Challege Cup ambayo yanadhaminiwa na Mbunge viti maalum Mkowa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati unazinduliwa rasmi kwa kwa timu kuanza kuchukua fomu za usajili kwa kulipa ada ya shilingi 50,000 na fomu zinapatikana katika kituo cha radio cha Nuru Fm.
Malekela alisema kuwa zoezi la uchukuaji fomu na kurudisha limenza rasmi tarehe 14 mwezi huu na litafikia kikomo tarehe 25 mwezi huu wa tano na baada ya hapo mchakato wa kupitia usajili na upangaji wa ratiba ya mechi itafanyika na baada ya hapo tunatarajia kuzindua rasmi tarehe 1 au 2 ya mwezi wa sita yaani mwezi ujao

“Fomu zinapatika kwa kamati wanaweza wakawasiliana na katibu kwa namba 0742483733 Au mwenyekiti Mimi hapa 0715779233 au wafike Nuru fm watapata na wale waliombali bado unaweza ukatumia fomu baada ya kutuma ada 50,000 tunakutumia mnajaza mnarejesha” alisema Malekela

Aidha Malekela alisema kuwa matarajio ya kamati msimu huu ni kuwa na timu chache ili kufanya vizuri katika mashindano hayo na makadilio kupata timu 40 kwa Mkoa mzima. Msimu wa mwaka jana tulikuwa na timu zipatazo 67 na kamati ilipambana na mashindano yakaisha bila kuwepo tatizo lolote licha ya kasolo ndogondogo ambazo ni udhaifu wa kibinadamu.

Malekela alisema kuwa lengo la mashindano ni kuibua vipaji vya vijana mkoani Iringa,Kuonesha uwezo wa vijana na kutengeneza ajira  kwao,Kujenga kizazi chenye afya bora na kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi,Kutoa burudani kwa wakazi wa iringa kwa  mchezo wa mpira wa miguu,Kuwakutanisha vijana pamoja ili kuzungumza lugha moja ya kimichezo na maendeleo,Kuwaepusha vijana na makundi au vijiwe visivyo faa na Kuhamasisha michezo katika mkoa wa Iringa,kutimiza agizo la makamu wa raisi juu ya kufanya mazoezi 
“Sasa hapo utagundua kuwa jinsi gani mashindano hayo yalivyo yanaumuhimu katika kukuza vipaji hapa mkoani kwa ustawi wa soka letu la nchi hiii” alisema Malekela
 Lakini Malekela alizitaja zawadi pamoja ambazo zitatolewa kwa timu shiriki

No.
Muhusika
Zawadi ya kwanza
Zawadi ya pili
1.   
Mshindi wa kwanza
Kombe 
2,000,000.00
2.  
Mshindi wa pili

1,000,000.00
3.  
Mshindi wa tatu

500,000.00
4. 
Mchezaji bora

100,000.00
5.  
Mfungaji bora

100,000.00
6. 
Golikipa bora

100,000.00
7.   
Waamuzi bora

100,000.00
8. 
Ushangiliaji bora

200,000.00
9. 
Timu yenye nidhamu

100,000.00

Jumla

4,200,000

Ligi yetu itakuwa kama msimu uliopita tutakuwa na hatua ya mtoano kulingana na timu zitakazo jitokeza kuchukua fomu za kushiriki mashindano haya na hatimaye kupata timu kumi ambazo zitacheza hatua ya makundi mawili na kupata timu nne ambazo zitacheza nusu fainali na hatimaye fainal
Kama kamati tunamshuru sana Mh.Mbunge Ritta Kabati kwa kukubali kudhamini mashindano haya na kuwathamini
vijana wa mkoa wa Iringa fedha hii ambayo anaitoa kwaajili ya kufanya yote haya angeitumia kwa kazi zake nyingine kwa maendeleo ya familia yake lakini kwa kutambua nafasi aliyonayo na kuwathamini vijana ndio maana anafanya haya yote hivyo sisi kamati tunamshukuru na kumpongeza aendelee kuwa na moyo huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.