Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Mei 17, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Mei 17, 2019 amefungua Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akiongozana na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Mkutano huo, kuingia kwenye ukumbi wa Simba kufungua Semina hiyo. Kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kicheere, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay na wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Musa Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Mei 17, 2019 amefungua Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akiongozwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Semina hiyo kuingia kwenye kukumbi wa Simba ili kufungua Semina hiyo. Kutoka kulia ni Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kicheere, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Musa Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Musa Nsekela wakati aliopowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kufungua Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, Machi 17, 2019. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, wa tatu kushoto ni Balozi wa Denmark nchini, Einar Hebogard Jensen na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Rota Sanare.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi baada ya kufungua Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Mei 17, 2019. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Musa Nsekela na wa tatu kushoto ni Balozi wa Denmark chini, Einar Hebogard Jensen.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment