Habari za Punde

ZAPSWU wadai malimbikizo ya nyongeza ya mishahara kisiwani Pemba

Na Masanja Mabula –Pemba
WANACHAMA wa Chama cha wafanyakazi ZAPSWU, kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar –ZAWA –Pemba wamewasilisha malalamiko yao kwa chama hicho wakidai kutolipwa aria zao za miezi kumi na  tano zinazotokana na nyongeza ya mshahara.
Malalamiko hayo yamewasiishwa na mmoja wa wanachama wa chama hicho, kwa Naibu Katibu Mkuu wa ZAPSWU,  katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Maktaba Chake Chake Pemba.
Amesema hichi ni kilio kikubwa cha wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuutaka uongozi wa ZAPSWU kulifanyia kazi ili waweze kupata haki zao.
“Hichi ni kilio cha muda mrefu kwa wafanyakazi wa ZAWA Pemba, kwani tunadai aria zetu  za miezi kumi na tano tangu Rais Shein alipotangaza nyongeza ya mshahara”alifahamisha.
Naibu Katibu Mkuu wa ZAPSWU , Suleiman Juma Suleiman amekiri kuwepo na changamoto hiyo kwa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.
Suleiman amesema taarifa hizo zilikifikia chama hicho, na kukutana na Uongozi wa ZAWA , lakini walitoa sababu za ndani na kuahidi kufuatilia.
“ZAPSWU inazo taarifa juu ya wafanyakazi wa ZAWA kutolipwa area zao, tumfuatilia na tunaendelea kufuatilia ili haki ipatikane”alisema.
Kisha akatoa wito kwa uongozi wa ZAWA Pemba kuhakikisha wanalipa , kinyume na hapo watalifikishwa ngazi za juu serikalini kwa hatua.
“Naiomba sana ZAWA kuwapa haki zao wafanyakazi, wakishindwa sisi kama chama tutalikisha serikali kwa hatua za kisheria”alisisitiza.
Amefahamisha moja ya majukumu ya vyama vya wafanyakazi ikiwemo ZAPSWU ni kusimamia na kutetea haki na naslahi ya wafanyakazi wanachama , na kwamba watahakikisha haki wazodai wafanyakazi wa ZAWA zinapatikana.
Mmoja wa maafisa wa ZAWA Pemba (jina tunalo) amesema suala hilo lipo nab ado halijapatiwa ufumbuzi, jambo ambalo limewaweka njia panda juu ya kupata stahiki zao hizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.