Habari za Punde

KMKM Wajiandaa na Tamasha la Siku ya KMKM Zitakazofanyikia Katika Uwanja wa Maisara Suleiman.

Na.Mwanajuma Juma.
KIKOSI Maalumu cha Kuzuia Magendo KMKM  kimejipanga kuhakikisha inaimarisha michezo yote ambayo yamo katika kikosi hicho.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Idara Maalumu za SMZ Khatib Ali Hamdu alipokuwa akizinduwa sherehe za kuadhimisha siku ya KMKM zilizofanyika katika viwanja vya  kikosi hicho viliyopo Maisara mjini hapa.

Alisema kuwa ingawa sio msemaji wa kikosi hicho lakini kwa kuanzia na hili la uzinduzi lililoandaliwa na timu ya KMKM ni dhahiri kwamba watafanya hivyo na kwa michezo mengine.

Alifahamisha kwamba yeye anachoelewa ni kwamba michezo ni mahusiano na hatua hii ya kushirikisha na wafanyakazi wengine inaimarisha mahusiano hayo.

Aidha alisema kuwa lengo kuu la kufanya siku hiyo kwa Timu hiyo ya KMKM ni kuwa  wanataka kuonesha kama KMKM ipo sambamba na kujitangaza wapi walipo na mambo gani wanafanya.

“Hakuna lengo jengine ambalo lipo isipokuwa ni hayo ambayo nimewaelezea na ni imani kwamba watafanikiwa”, alisema.

Jumla ya timu nane zinashiriki katika bonanza hilo la Michezo ikiwemo Timu ya Wizara ya Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mafunzo Veteran, Polisi Veteran, Zimamoto Veteran, JKU Veteran, KVZ Veteran, Bandari na wenyeji KMKM Veteran, ambapo kilele chake kitafikia Julai Mosi mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.