Habari za Punde

Othman Abdalla Foreman na Said Ibrahim Njuju Kuelekea Nchini Misri Kuangalia Michuano ya Fainali ya AFCON.

Waziri wa Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar Mhe. Balozi Ali Abeid Karume, akiwa na Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar kulia Othman Abdalla Formen na kushoto Said Ibrahim Njunju, akiwazungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wakati wa kuwaaga wakielekea Nchini Misri kushuhudia Michuano ya Fainali ya Afcno.

Na. Mwajuma Juma.
WAZIRI wa Wizara ya Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo Balozi Ali Karume amesema Wizara inathamini kwa  kiasi kikubwa mchango wa wachezaji wa zamani ambao walitamba na kuiletea sifa nchi yao.

Balozi Karume aliyaeleza hayo usiku wa kuamkia jana Waziri huyo alitoa pongezi hizo hapo usiku wa Jana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa  Abeid Amani Karume katika hafla ya kuwaaga wachezaji Othman Abdalla Fomen na Said Ibrahim Njunju ambao wanakwenda nchini Misri kwenda kuishangilia timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars katika Michuano ya AFCON Cairo nchini Misri inayoanza kutimua vumbi jana.

Alisema kuwa kwachezaji hao ambao mbali ya kuvitumikia vilabu vyao waliweza kutumikia nchi kwa miaka mingi kupitia timu ya Taifa na kutamba na hata kutengeneza majina makubwa. 

Hivyo alitumia fursa hiyo kuzipongeza  shirikisho la Soka Zanzibar ZFF pamoja na Taasisi ya "MIMI NA WEWE" kwa kuwasafirisha wachezaji hao kitendo ambacho alikisemea kuwa kinawafanya wachezaji kujiona kuwa nao wanakumbukwa kwa mchango wao.

“Wachezaji wa zamani wapo wengi na hivyo ni vyema kukumbukwa kupitia harakati zao za Soka walizozifanya miaka ya nyuma ambao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kulitangaza Soka la Zanzibar ndani na nje”, alisema. 

Aidha aliwataka wachezaji hao kushirikiana na Watanzania waliopo huko Misri katika kuipa hamasa timu Yao ya Taifa stars Ili iweze kufanya vizuri zaidi kwani uwezo wa kufanya hivyo wanao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya "MIMI NA WEWE" ambae pia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud alisema fursa hiyo ya kuwaenzi wachezaji wa Zamani itaendelea kutolewa na taasisi yake iIli kuhakikisha wanarejesha hamasa kwa Mashabiki wa Soka na hata wachezaji kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Alifahamisha kwamba  wameanza na wachezaji hao wawili kwa kwenda kushuhudia AFCON hivyo wachezaji wengine wazamani pia watapata fursa ya kushuhidia Michuano mingine ambayao timu za Taifa zitakaposhiriki. 

Nae Rais wa ZFF Seif Kombo Pandu aliwataka wachezaji hao wa Zamani kuwa na mashirikiano ya karibu na shirikisho hilo na hata kuwapa ushauri pale wanapohitaji kwa mustakabali wa kukuza na kuliendeleza Soka la Zanzibar.

Awali katika safari hiyo ilimuhusisha mchezaji wa zamani Seif Nassor Bausi lakini haikuwezekana kutokana na kile kilichodaiwa kukosa baadhi ya nyaraka muhimu za kusafiria na nafasi yake kuchukuliwa na Said Ibrahim Njunju.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.