Habari za Punde

PSSSF Yawahakikishia Wanachama na Wastaafu wa Mfuko Huo Kwa Huduma Bora za Haraka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayoub Ryoba (kushoto), akiwa kwenye mazungumzo na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, wakati meneja huyo alipotembelea studio za TBC Mikocheni jijini Dar es Salaam Juni 12, 2019. Ziara hiyo ilikuwa ni muendelezo wa ziara ya Bi. Chiume kutembelea vyombo vya habari jijini ili kuimarisha mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo ambao ni mpya. PSSSF iliundwa baada ya kuunganishwa kwa Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF. Vyombo vingine ambavyo PSSSF ilivitembelea katika ziara ya Juni 12, 2019 ni pamoja na Kampuni ya Uhuru Publications Limited (UPL), Kampuni ya African Media Group, wamiliki wa Channel Ten na Magic FM, kampuni inayochapisha gazeti la Jamhuri, Kampuni ya New Habari (2006) wachapishaji wa magazeti la Mtanzania, Rai, na Dimba. Pamoja na mambo mengine, Meneja huyo kiongozi amesema Mfuko umeanza kutekeleza majukumu yake Agosti 1, 2018 na kwamba uko imara na kuwahimiza wastaafu wajitokeze kwa wingi katika zoezi la kuhakiki taarifa zao ili kuondoa usumbufu wakati wa kufanya malipo ya pensheni na kutoa hakikisho la kupata huduma bora na za haraka.
 Bi. Eunice Chiume akiwa na Mkurugenzi wa Chaneli ya kitalii ya TBC Safari Channel, Bw. Gabriel Nderumaki (wapili kulia), wakati akiangalia studio inayotembea yaani OB VAN ya kisasa kabisa ya shirika hilo. Gari hilo maalum ambalo limefungwa mitambo na kufanyab studio kamili huwezesha matangazo ya moja kwa moja na lina uweso wa kusafiri mahapa popote hapa nchini. Anayetoa maelezo ni mtaalamu wa ufundi na mitambo wa TBC Bw. K.A Chitenda.
 Studio ya kusomea taarifa ya habari TBC.
 Picha ya pamoja na uongozi wa TBC
 Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume akizungumza wakati alipotembelea ofisi za New Habari Sinza jijini Dar es Salaam
  Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume akizungumza na uongozi wa kampuni ya New Habari Sinza jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Uhusiano Mwanzamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi na kulia kwake ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Denis Msacky.
 Picha ya pamoja na uongozi wa New Habari(2006) 
 Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Publications wachapishaji wa magazeti ya Cham cha Mapinduzi (CCM), Uhuru na Mzalendo, Bw. Kiondo Mshana (kushoto), akibadilishana mawazo na Meneja Kingozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, wa PSSSF Bi. Eunice Chiume, (kulia) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, wakati Meneja huyo alipofanya ziara kwenye ofisi za kampuni hiyo Juni 12, 2019.

Mhariri wa gzeti la Uhuru, Bw. Ramadhan Mbwaduke, akisalimiana na Bi. Eunice Chiume alipotembelea ofisi za gazeti hilo Juni 12, 2019
 Bi Eunice Chiume akipo ngozana na Mhariri wa gazeti la Jamhuri, Bw.
 Picha ya pamoja na wafanyakazi wa gazeti la Jamhuri.
 Bi. Enice Chiume akisalimiana na Mhariri wa Channel Ten, Bi. Dina Chahali.
Bi. Eunice Chiume akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSS, Bw. Abdul Njaidi, wakisalimiana na Meneja Uendeshaji wa AMG, Bw.Elias Shamte.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.