Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk A\Shein Akiwasili Viwanja Vya Sheikh Idrissa AbdulWakil Kikwajuni Zanzibar.

Msafara wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, ukiwasili katika viwanja vya Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, kuhudhuria hafla ya Baraza la Eid Fitry baada ya kumalizika kwa mfungo wa  mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuandama kwa mwezi jana. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar ,kuhudhuria Baraza la Eid Fitry leo. 
Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dkt.Amani Abeid Karume akisalimiana na Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar Mhe. Khamis Juma Maalim alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishin Kikwajuni kuhudhuria hafla ya Baraza la Eid Fitry leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil Kikwajuni Zanzibar leo kuhudhuria hafla ya Baraza la Eid Fitry.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akielekea katika ukumbi baada ya kuwasili katika Viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar kuhudhuria hafla ya Baraza la Eid Fitry Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohamed Shein, akipokea saluti kutoka kwa gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili ya Baraza la Eid Fitry na Kikosi cha FFU katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.  


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.