Habari za Punde

Maofisa Mawasiliano Elimu na Tehama Watakiwa Kujenga Mahusiano na Taasisi za Habari.

Katibu Mkuu Wizara Katiba na Sheria Ndugu George Joseph Nazi na Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Bi Daima Mkalimoto katika kikao na Maafisa Habari mawasiliano na Elimu wa Wizara hiyo. 
Katibu Mkuu Wizara Katiba na Sheria Ndugu George Joseph Kazi  wakati wa kikao cha pamoja na Maafisa Habari Mawasiliano na Elimu  na Maafisa Tehama kutoka Taasisi mbali mbali zilizopo ndani ya Wizara ya Katiba na Sheria kwenye ukumbi wa Mkutano Mazizini.

Na Raya Hamad – WKS
Maafisa wa habari, Tehama, elimu na mawasiliano wa  Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kujenga mahusiano na  mashirikiano  baina yao ili kuwepo utekelezaji mzuri wa majukumu na ufanizi katika  kazi zao

Katibu Mkuu Wizara wa  Katiba na Sheria Ndugu George Joseph Kazi ameyasema hayo wakati alipokutana na maafisa habari  na mawasiliano , Elimu na Tehama kutoka taasisi zilizomo ndani ya wizara hio katika ukumbi wa Mkutano Mazizini

Ndugu George amesema majukumu ya Wizara  hayaitakiwi kutekelezwa kimya kimya bali  kinachotakiwa wananchi waelewe na wafahamu huduma zinazotolewa katika taasisi hizi kwa kutumia Website ya Wizara na zile zilizomo ndani ya taasisi , vyombo vya habari vikiwemo televisheni gazeti , redio, majarida, vipeperushi na mitandao ya kijamii kama  Tweeter, Facebook, Youtube nk  ili kuitangaza na kuisemea Wizara .

Aidha amewataka maafisa hao kutojibebesha majukumu ambayo hayaendani na majukumu yao ya kazi kwani kufanya hivyo kutapelekea kujinyima haki zao za msingi kwa vile hivi sasa mfanyakazi anapimwa namna ya utendaji wake wakazi

Ametolea mfano kwa sekta ya sheria na kusema kuwa wananchi wengi hawana uwelewa juu ya namna ya kutafuta haki na wengine wanakiuka sheria bila kufahamu hivyo vitengo vya habari vya taasisi za sheria wanalo jukumu la kuandaa na  kuihabarisha jamii kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi hizo, Wananchi wanataka kufahamu vitu vingi kutoka Wizara hii ambayo imekusanya tasisi muhimu ndani yake

Katika kulifanikisha hili George amewataka maafisa hao kuwa na mtandao wa pamoja  utakaoweza kurahisisha, kukuza na kuimarisha mawasiliano ya habari kati ya  kitengo cha Habari cha Wizara na vitengo vya habari,  mawasiliano na elimu na Tehama ambavyo vimo ndani ya Taasisi za Wizara zikiwemo Tume ya kurekebisha Sheria, Idara ya Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Ofisi ya Mufti, Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana.

“Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, sekta ya sheria kimsingi imezungumziwa kuziimarisha na kuhakikisha inatekeleza wajibu wake  mategemeo ya Wizara kupitia kikao hiki mtatengeneza mtandao imara kati yenu ambao utakuwa ni chachu ya kuleta mafanikio  yatakayopelekea  Jamii kufahamu huduma zinazotolewa na Wizara kupitia Taasisi zetu”amesisitiza Gearge Kazi

Nae Mkurugenzi wa mipango Sera na Utafiti Bi Daima Mohamed Mkalimoto amewataka maafisa kuwa wabunifu kwani wizara ya katiba na sheria ndio msimamizi wa sera kwa masuala yote wanayoyasimia hivyo ni makosa kuona majukumu na huduma zinazotolewa  wanachi hawazielewi .

Hata hivyo amewataka maafisa hao kutoa taarifa sahihi  kuwa makini pamoja  na kufuata muongozo na maelekezo kutoka kwa wakuu wao wa kazi ili taarifa zitakapotoka ziendane na uhalisia wa habari zenyewe

Nao maafisa hao wameahidi kutekeleza kwa vitendo na kuweka mikakati ya pamoja ya kiutendaji kwa kufanya kazi kwa mashirikiano  na kuhakikisha habari zinawafikia wananchi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuandaa vipindi maalum na makala .

Lengo la kikao hicho  ni kujadili namna bora ya kuimarisha mashirikiano na uhusiano wa kiutendaji,   kupanga mikakati ya pamoja na kujadili  changamo zilizomo kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Elimu wa Wizara ili kuleta ufanisi na kuitangaza vyema Wizara ya Katiba na Sheria na hatimae wananchi waweze kufahamu na kuelewa utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo  .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.