Habari za Punde

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KATIKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO-ZANZIBARTume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Fedha na Mipango kama ifuatavyo:-


1. Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

2. Msaidizi Fundi Umeme Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Cheti katika fani ya Ufundi wa Umeme kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Msaidizi Fundi Bomba Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehimu elimu ya Cheti katika fani ya Ufundi Bomba kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Afisa Habari Daraja la II “Nafasi 1” Pemba 
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya “Mass Communication” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Afisa Takwimu Daraja la II “Nafasi 2” Unguja na “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Takwimu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Afisa Uchumi Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi au Mipango kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7. Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango na Sera kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

8. Mkaguzi wa Ndani wa Serikali Daraja la II “Nafasi 5” Unguja
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uhasibu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

9. Afisa Uhakikimali Daraja la II “Nafasi 4” Unguja 
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Ununuzi na Ugavi’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

10. Afisa Kumbukumbu Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

11. Afisa Usafiri Daraja la II “Nafasi 2” Unguja
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Usafiri kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

12. Afisa Hifadhi ya Jamii Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Hifadhi ya Jamii (Social Protection) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


13. Afisa Bima Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Insurance and Risk Management kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

14. Microfinance Officer Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Microfinance and Community Economic Development kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

15. Finance and Banking Daraja la II “Nafasi 3” Unguja
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Banking au Uhasibu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

16. Afisa Mitaji ya Umma Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Fedha au Fedha na Uwekezaji kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

17. Afisa Mtathmini Mali Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Land Management and Valuation kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587,
ZANZIBAR.
Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 31 Julai, 2019 wakati wa saa za kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.