Habari za Punde

TCRA Yatowa Elimu kwa Masheha wa Wilaya ya Mjini na Magharibi Unguja.

Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Zanzibar Bi. Mtende Hassan akitowa maelezo ya Utumizi Salama wa Mitandao wa Simu kwa Masheha wa Wilaya ya Mjini na Magharibi Unguja, akionesha Kitabu cha Mkataba wa Huduma Kwa Mteja wa TCRA, wakati wa Mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi B Unguja Mombasa. 

Na Hawa Ally. ZANZIBAR 
MAMLAKA ya mawasiliano TCRA Ofisi ya Zanzibar imetoa mafunzo kwa baadhi ya masheaha wa Mkoa wa Mjini Magharibi kwa lengo la kuwapatia elimu juu ya usajili mpya wa alama za vidole katika maeneo yao.

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika katika ukumbi wa Almashauri ya wilaya ya Magharibi B hapa Unguja.

Akiwasilisha Mada katika mafunzo hayo Mhandisi wa TCRA Ofisi ya Zanzibar Mtende Sherazi Hassan amewataka masheaha kuwa mabalozi wazuri wa kuwahamasisha Jamii kusajili laini zao kwa wakati kupitia njia ya alama za vidole Ili kukabiliana na vitendo vya kiharifu wa mitandao. 

Alisema masheaha wawe makini na mawakala wanaosajili laini kupitia alama za vidole mitaani kwa kuwatoza watu fedha kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria badala yake wawe na ofisi maalum ambazo zinatambulika kisheria.

Alisema baadhi ya wanaosajili laini mitaani au nyumba kwa nyumba sio waaminifu huku wengi wao wakijihusisha na utapeli wa mitandao kwa kuhamisha miamala ya fedha katika simu ya anaempatia huduma hiyo ya usajili.

"Wapo wanaosajili laini wanajihusisha na utapeli wa mitandao hususani wa miamala ya fedha maarufu tuma kwa namba hii, wananchi wawe makini sana" Alisema.

Hata hivyo amewataka wananchi wanapopata tatizo kuacha kunung'unika na badala yake wapeleke malalamiko yao katika mamlaka husika.

Nae mkaguzi wa polisi kutoka kitengo cha makosa ya mtandao kutoka  jeshi la Polisi Issa Mohammed Salum akiwasilisha  Mada ya makosa ya mitandao aliwataka wananchi kuepuka kununua simu mkononi kwani simu hizo nyingine zimefanyiwa uhalifu wa kimtandao.

Alisema Mara nyingi wahalifu wanapotekeleza tukio hutupa ushahidi hivyo kununua simu hizo inaweza kuwaletea matatizo makubwa kwani huwenda uharifu huo unaweza kuwa wa mauwaji au utapeli mkubwa wa mamilioni.

Aidha Aliwataka wananchi wanaopoteza laini zao au simu zao kuripoti kituo cha polisi kwani kutofanya hivyo uwende laini hiyo inaweza kufanyiwa uhalifu bila mwenyewe kujua na mwisho wa siku ukajikuta mkononi mwa polisi. 

"unapopoteza laini fika kituo cha polisi kutoa taarifa, kukaa kimya pia ni Kosa kwani hujui aliyeiyokota atafanyia kitu gani anaweza kutapeli watu halafu ikifuatiliwa usajili unakutwa jina lako na hatua ya Kwanza ya uchaguzi lazima uanzie kwao wewe".Alisema

Kwa Upande wa Masheaha waliopata elimu hiyo ya usajili wa laini wamelupongeza jeshi la polisi kupitia mamlaka ya mawasiliano kwa kutoa elimu hiyo kupitia ujumbe mfumpi wa maandishi ambao wananchi wengi wa au pokea. 

Kwa Pamoja walisema elimu hiyo wataifikisha katika mashehia yao kupitia kamati za shehia ili kutoa taadhari kwa waharifu wa mitandao kumtumia fursa hiyo ya kusajili Lani majumbani jambo ambalo ni kose kwa sheria za TCRA. 
Jumla ya laini milioni 43 zimesajiliwa huku laini milioni 20 zinatumika kwa huduma za kifedha

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.