Habari za Punde

Uchunguzi wa Awamu ya Pili ya Saratani ya Shingo ya Kizazi Kwa Wanawake Wafanyika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja


Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Uchunguzi na Utibabu wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake inayofanywa na madaktari Kutoka China Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Mmoja kati ya madaktari kutoka China Hupaohai akifanya uchunguzi wa maradhi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Mmoja kati ya madaktari wanaoshirikiana na Madaktari kutoka China Faiza Habibu (kushoto)akimfanyia mahojiano Mwananchi Zuhura Bazi Mkaazi wa Chukwani katika uchunguzi wa maradhi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano  uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Uchunguzi na Utibabu wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake inayofanywa na madaktari Kutoka China Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano  uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.kulia ni Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman.  
Mwakilishi Nafasi za Wanawake Panya Ali Abdalla akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufanyiwa Uchunguzi  wa maradhi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed(katikati) na Naibu Waziri wa Afya  kushoto yake wakiwa katika Picha ya pamoja na Madaktari Kutoka China waliofika Nchini kwa ajili ya kufanya Uchunguzi na Utibabu wa  Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake uliofanyika Hospitali Mnazi Mmoja Zanzibar. 

Na Kijakazi Abdalla.-Maelezo  Zanzibar.  01/7/2019.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed amesema kuwa kuwepo kwa zoezi la uchunguzi wa saratani ya kishingo ya kizazi ni kuweza kupata takwimu sahihi ya kujua wanaosumbuliwa na maradhi hayo hapa Zanzibar.
Hayo ameyasema huko katika Hospitali ya Mnazi mmoja  wakati akiangalia zoezi zima la uchunguzi wa saratani wa shingo ya kizazi kwa wanawake.
Amesema kuwa kwa hivi sasa idadi kamili bado haijulikani kwa wanaousumbuliwa na maradhi hayo jambo  linaifanya kuweza kutoa takwimu sahihi na hata maeneo gani yaliaathirika na maradhi hayo.
Aidha alisema kuwa kupata takwimu sahihi pia kutawezesha Wizara ya Afya kuengeza bajeti ya tiba ili kuweza kurahisisha na  kupambana na maradhi hayo.
Aidha alisema kuwa maradhi ya  saratani ya shingo ya kizazi yanatibika bila ya hata kwenda kwa waganga kwani  tiba sahihi ya maradhi  hayo yanapatikana katika hospitalini.
Alisema kuwa kinamama walio wengi  wamekuwa wanaamini kuwa ugonjwa huo unatokana na kurogwa jambo ambalo sio sahihi hali ambayo inaweza kutowafanya kutofika hospitali kwa ajili ya uchunguzi.
“Kinamama wengi mnaamini maradhi haya yanatokana na kurogwa na hasa wale  wanawake wenye  wakewenza kumbe sio sahihi”, alisema Waziri Rashid.
Hata hivyo amewataka kinamama kujitokeza kwa wengi katika vituo vya afya kuchunguza afya zao ili kuweza kujua hali zao mapema jambo ambapo litaweza kuondokana na usumbufu mara wanapobainika wanasumbuliwa na maradhi mbalimbali.
Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikijitahidi kupambana na maradhi mbalimbali hali kwa wananchi wake ili kuweza kupata taifa lenye afya.
Nae Mratibu wa Mradi wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi kutokana Serikali ya Jamuhuri ya watu wa China QI Xiaomin amesema kuwa zoezi la kufanyia uchunguzi kinamama linafanyika kitaalamu kwa hali ya juu kabisa.
Nae Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyoambikiza Zanzibar Omar Mwalimu Omar  amewataka kinamama kuitumia fursa iliyowepo ili kuweza kupatiwa vipimo kwa uhakika.
Hata hivyo alisema uzuri wa kupatiwa vipimo kwa uhakika kutawezesha kinamama kuondokana na kutumia gharama nyingi za matibabu pale wanapobainika na maradhi kama hayo.
Nae Mwakilishi wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Kaskazini Panya Ali Abdalla ambae alishiriki katika zoezi la uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa kuazisha zoezi hili .
Aidha aliwataka kinamama kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili kwani halina malipo wala halina usumbufu kwa wale wanasumbuliwa na ugonjwa huo na tiba yake inapatikana .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.