Habari za Punde

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Mwakiembe Azindua Mbio za Capital City Marathon Jijini Dodoma leo.

 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (aliyeshika filimbi nyekundu) akionyesha ishara ya kuanza kwa mbio za Capital City Marathon kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluh Hassan zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.
Baadhi ya wanariadha walioshiriki mbio za Capital City Marathon wakijiandaa kuanza mbio zilizofanyika leo
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Bw.Rashid Ally baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za Baiskeli Km.22 za Capital City Marathon zilizofanyika leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Bw.Godlisten  Mmary  baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za walemavu za Capital City Marathon zilizofanyika leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Bw.Emmanuel Giniki  baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za Km. 21 kwa wanaume za Capital City Marathon zilizofanyika leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Bi.Fabiola John  baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za Km. 10 kwa wanawake  za Capital City Marathon zilizofanyika leo Jijini Dodoma.Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Mhe.Antony Mavunde.
Mratibu wa Mbio za Capital City Marathon Bw.Nsolo Mlozi akitoa neon la shukrani kwa washiriki wa mbio hizo  zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.Kulia ni  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe(Katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa mbio za Capital City Marathon kwa upande wa walemavu pamoja na viongozi wa Mkoa,Chama  na Serikali baada ya kumalizika kwa mbio hizo zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.