Habari za Punde

Malindi yaambulia sare na Mogadisho City kombe la Shirikisho


Na Mwandishi Wetu, 

WAWAKILISHI wa Zanzibar kwenye Kombe la Shirikisho, Malindi SC nao wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mogadishu City ya Somalia katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya kwanza jioni ya leo Uwanja wa Amaan.

Sasa Malindi watajaribu tena bahati yao katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Zanzibar pia wiki ijayo kwa ombi la wageni na mshindi atakutana na mwakilishi wa Misri.

Matokeo hayo yanakuja siku moja baada ya jana, KMKM SC kuchapwa 2-0 na Primiero de Agosto ya Angola katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Amaan.

Timu hizo zitarudiana wiki ijayo mjini Luanda na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Green Eagles FC ya Zambia na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.