Habari za Punde

Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar atembelea Shirika la Posta jijini Dar

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), akimkaribisha Waziri Dkt. Sira Mamboya kuzungumza na uongozi wa shirika. 
Postamasta Mkuu wa Shirika la PostaTanzania (TPC),
Hassan Mwang'ombe (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya (katikati), alipotembelea shirika hilo, Makao Makuu, jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa waziri Mamboya ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Mh.Mhandisi Atashasta Nditiye (Mb) na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali mstaafu, Dkt. Haruni Kondo.
Meneja Mkuu wa Shirika la Posta, Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo, akitoa maelezo kuhusu shirika hilo, lilikotoka hadi sasa na malengo yake ya baadaye kwa Waziri Dkt. Sira Mamboya, wakati wa ziara hiyo.
Waziri Dkt. Sira Mamboya (wapili kulia), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (watatu) na Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, wakimsikiliza Meneja Mkuu Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo. 
Meneja Mkuu wa Shirika la Posta, Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo, akitoa maelezo kuhusu shirika hilo.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Meneja Mkuu, Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), kumkaribisha Waziri Dkt. Sira Mamboya (wapili kushoto) kuzungumza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya, akizungumza na uongozi wa Shirika la Posta, jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri Dkt. Sira Mamboya (katikati), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (watatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Shirika la Posta. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali mstaafu, Dkt. Haruni Kondo na wa pili kulia ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe. 


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya, akiagana na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye mara baada ya kumaliza kupiga picha ya pamoja katika ziara hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.