Habari za Punde

Moto wateketeza maduka Stendi Kuu ya Chakechake

 Askari wa kikosi cha Zimamoto Kisiwani Pemba, wakishiriki kuzima moto wakati moto ukiunguza maduka ya wafanyabiashara wa maeneo ya Stand kuu ya Chake Chake Pemba,
 Maofisa wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Pemba, wakimsaidia Askari wao kuvaa Mtungi wa gesi kwa ajili ya kuwahi kuzima moto ambao ulikuwa unatetekeza maduka katika eneo la Stand ya Chake Chake Pemba.
  Maofisa wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Pemba, wakimsaidia Askari wao kuvaa Mtungi wa gesi kwa ajili ya kuwahi kuzima moto ambao ulikuwa unatetekeza maduka katika eneo la Stand ya Chake Chake Pemba.Askari wa kikosi cha Zimamoto na uokozi Pemba , wakisaidia kutowa Sanduku linalodaiwa kuwa na fedha ambazo zilishaanza kuunguwa wakati moto ukiteketeza maduka huko katika eneo la Stendi ya chake Chake


-Pemba.
PICHA NA BAKAR MUSSA-PEMBA.


 Askari Polisi katika Wilaya ya Chake Chake Pemba, wakisaidia kuvunja sanduku ambalo lilikuwa linateketea kwa moto ili kuokowa baadhi ya fedha ambazo zilikuwa zinaunguwa huko katika eneo la stand ya Chake Chake Pemba.
Baadhi ya pesa za noti na sarafu ambazo baadhi yake zilikwisha unguwa zikiwa zimetolewa katika sanduku ambalo lilikuwa limeshaanza kuteketea kwa moto huko katika eneo la stand ya Chake Chake Pemba.Magari ya kikosi cha Zimamoto na uokozi Pemba, yakiwa katika katika harakati za kuzima moto ambao ulikuwa unateketeza baadhi ya maduka yaliopo katika eneo la Stand ya Chake Chake Pemba.PICHA NA BAKAR MUSSA -PEMBA.


 Wafanyakazi kutoka Zimamoto na Uokozi  wakionyesha jihitada ya kuzima moto uliyoteketeza baadhi ya maduka katika Soko kongwe la Mbogamboga lililopo Chake-chake Kisiwani Pemba 
Wananchi wa Chake-chake wakishuhudia Moto ukizimwa katika  baadhi ya Maduka yaliyoteketea kwa moto katika Soko kongwe la mbogamboga lililopo Chake-chake Kisiwani Pemba.


           Picha Na Miza Othaman –Maelezo Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.